Sunday 26 May 2013

KABLA HATUJASAHAU YALIYOTOKEA HUKO KISII KENYA, SASA NI TANZANIA, VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA. HIVI KWELI TUMEFIKIA HAPA?


MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina. 

 Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.


 Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo ambaye alifariki kwa ajali ya pikipiki hivi karibuni, na kwa mujibu wa ndugu wa marehemu huyo, mzimu wa  marehemu  umekuwa ukiwajia usiku mara kwa mara, hali ambayo ilipelekea kuwa na imani za kichawi.
Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!