Wadau,mazuri ayafanyayo huyu binti hayasemwi ila mabaya yake tu.Wema amefanya vitu vingi vikubwa na vizuri ila watu wanasemea chinichini tu na si wengi wamempongeza hadharani.Hii inamaanisha wengi hawafurahii mafanikio yake.
Kumbukeni kuwa mtoaji ni Mungu na kamwe Mungu akitia mkono wake katika maendeleo ya mtu mwanadamu huwezi kubadilisha kitu.Walaaniwe wale wote wanaotaka kumkatisha tamaa binti huyu kwa namna yoyote ile.
Wema ziba masikio na endelea kufanya yale uliyodhamiria.Wengi wanataka kuwa kama wewe ila hawawezi na hiyo ndiyo sababu ya wao kutaka kukukatisha tamaa ili urudi chini na kuwa kama wao.
USHAURI KUTOKA SOPHIE BLOG:Wema unaweza hivyo usikatishwe tamaa na kiumbe yeyote chini ya jua.Endelea kumwomba Mungu kwani yeye pekee ndiye hatakuacha. GO WEMA!GO!
Baadhi ya picha mbalimabli za Wema
No comments:
Post a Comment