Saturday 20 April 2013

NI UNYAMA GANI HUU?

Watanzania huyu ni binadamu mwenzetu ambaye leo alfajiri ya kuamkia leo Aprili 20 amekutwa na mauti.Sisi wakazi wa Mtaa wa Sinza 'C' eneo la Ukuta wa Posta  maarufu kama ukuta wa Kesi ya Abdallah Zombe, leo saa 11 alfajiri tulijikuta tukiamkia kuona mwili wa marehemu huyo ukivuja damu katikati ya barabara na ukiwa umelazwa chini baada ya kuua na watu wasiyojulikana.Nikiwa kama raia mwema na Mwandishi wa habari baada yakufika eneo hilo la tukio nilichofanya nikumpigia Simu mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala,ACP-Duwani Nyanda na Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Kinondoni, ACP- Charles Kenyela kuwapa taarifa na kweli baada ya muda mchache waliwaagiza askari wao wakafika eneo la tukio na kuuchukua mwili huo ambao ulikuwa unavuja damu.Inasikitisha sana, na inaendelea kudhiirisha kuwa baadhi ya watanzania hivi sasa wamezidi kuwa na roho katili na hawana hofu ya mungu.(Picha na Happiness Katabazi)
Mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika amekutwa na mauti usiku wa kuamkia leo April 20  katika hali ya kutatanisha.
 kwa mujibu wa wakazi wa Mtaa wa Sinza 'C' eneo la Ukuta wa Posta maa...rufu kama ukuta wa Kesi ya Abdallah Zombe, leo saa 11 alfajiri walipoamka walikuta mwili wa marehemu huyo ukivuja damu katikati ya barabara na ukiwa umelazwa chini baada ya kupigwa vibaya na watu wasiyojulikana.  Mwandishi wa habari ambaye alifika katika eneo hilo la tukio  alitoa taarifa  kwa mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala,ACP-Duwani Nyanda na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP- Charles Kenyela kuwapa taarifa ambapo baada ya muda mchache polisi walifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili huo ambao ulikuwa bado ukivuja damu.Inasikitisha sana, na inaendelea kudhiirisha kuwa baadhi ya watanzania hivi sasa wamezidi kuwa na roho katili na hawana hofu ya mungu alisema mwandishi huyo.
 
habari na kwa hisani ya Happiness Katabazi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!