Wednesday 17 April 2013

AIBU ZA WASANII WETU,NINI KIFANYIKE KUKOMESHA HILI


Diamond Platnumz

Irene Uwoya

Haya jamani,leo ngoja tuzungumzie swala la hawa wasanii wetu.Kama ambavyo tumesoma katika vyanzo tofauti kuwa msanii wa bongo flava  Naseeb au Diamond Platnumz na msanii wa Bongo movies Irene Uwoya ambae ni mke wa mtu(Hamad Ndikumana), walionekana wakiingia katika hoteli saa mbili za usiku na kutoka siku inayofuata saa nane mchana.Wasanii hao walichukua chumba kwa maana hiyo walilala hapo.
Kwanini Sophie Blog imeamua kuleta mjadala juu ya swala hili?Tunajua kuwa kuwa hawa wote kama wasanii ni kioo cha jamii, hivyo wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na jamii.Kwa haya wanayoyafanya kama ni kweli,tunajifunza nini?
Wote wawili wana makosa kama swala hili ni kweli .Tukianza na Irene,huyu ni mtoto, mama na mke.Kwa kufanya UCHAFU huu ameidhalilisha familia yake(wazazi),mwanae,mumewe,wasanii wenzie wa Bongo movies pamoja na washabiki wake-AIBU.
Tuje kwa Diamond Platnumz.Huyu nae labda kaingia katika fani kwa pupa kwani toka apate umaarufu amekuwa ni mtu wa vituko tu.Kwanini ameamua kuwadhalilisha wasanii wa kike kiasi hiki?Amefanya kitu kibaya sana kutembea na mke wa mtu,masikini Ndikumana.

Swali kwa Diamond,hivi ingekuwa ni mkewe ametolewa gazetini akiwa amekwenda kulala katika hoteli na bwana mwingine angejisikia vipi?Swali lingine kwake je ,hajui kama Irene ni mke wa mtu?Amelewa umaarufu hajui kuwa anaweza akapoteza umaarufu wote kwa siku moja?
Diamond,wewe ni kioo cha jamii,achana na uchafu unaofanya.Usiishi kilimbukeni kwani utaharibu jitihada zako zote katika muziki.
Haya,kabla hili halijakwisha,umeonyesha jinsi gani ulivyokuwa hujastaarabika kwa kurekodi maongezi yako  katika simu kati yako na  Wema.

Diamond,una mengi ya kujifunza vinginevyo jamii itakuchukia badala ya kukupenda. Punguza pupa na ulimbukeni.Kuna wasanii wengi WAKUBWA ambao umewakuta katika GAME na hawana makuu.Hatuhitaji kuwataja kwani unawajua.Unajua ni nini siri ya wao kuwa juu muda wote huo?NIDHAMU NA UNYENYEKEVU KWA JAMII.

Kama unasikia na usikie!

Mwito kwa watanzania:Sasa umefika wakati wa kuwapa mafunzo wasanii wenye utovu wa nidhamu kama wanavyofanyiwa nchi nyingine.Tunaweza kuwaadabisha kwa KUGOMA KUINGIA KATIKA MAONYESHO YAO NA KUACHA KUNUNUA KAZI ZAO!!

Je wasomaji wetu,nini maoni yenu katika hili?Changia kwa uhuru bila matusi tafadhali.


HEBU MDAU ANGALIA VIDEO HII


2 comments:

Anonymous said...

wasanii wetu wa bongo,miyeyusho tu huyu diamond heshima kwa dada zetu hana kabisa





mdau USA.

Anonymous said...

jamaa mshamba sana, ki muziki anajitahidi, lakini dogo anavamia mambo kwa pupa

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!