Wednesday 13 March 2013

MWANAMICHEZO WA WIKI-USAIN ST.LEO BOLT



Usain St Leo Bolt anajulikana kama ni mtu mwenye kasi zaidi (ya kukimbia) kuliko wote duniani.
Usain Bolt alizaliwa  Trelawny, Jamaica

Wazazi wa Usain Bolt ni  Wellesley na Jennifer Bolt Usain Bolt ana kaka aitwaye Sadiki na dada aitwae Sherine.Mchezo wa kwanza kumvutia Bolt ni kriketi, Vilevile Bolt anapendelea mpira wa miguu na ni shabiki mkubwa wa timu ya Manchester United.

Usain Bolt amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya Olimpiki kushinda  kwa pamoja mbio za mita  100 na mita 200 katika rekodi ya dunia mwaka 2008. Miaka minne baadaye, katika michezo ya Olimpiki ya London, akawa mtu wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki mita 100 na 200   mfululizo na mtu wa kwanza katika historia ya kuweka rekodi tatu  za dunia katika mashindano yaSingle Olympic Games.

Je,unajua Usain Bolt amesaini makubaliano gani na kampuni ya magari ya Nisaan?
Bofya hapa kufahamu      



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!