Friday, 15 March 2013

ZIMBABWE YAKATAA WAANGALIZI WA KIMATAIFA

Marekani inaisihi  serikali ya Zimbabwe  kuruhusu waangalizi wa kimataifa katika kura ya maoni ya Jumamosi juu ya katiba mpya.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Viktoria Nuland anasema watu wa Zimbabwe wamekuwa wakingoja kwa muda mrefu sana demokrasia  zaidi. Amesema kuruhusu wote waangalizi wa kimataifa na wale kutoka Zimbabwe ndio njia bora ya kuhakikisha hadhi ya  kura hiyo.

Zimbabwe imezuia waangalizi kutoka nchi za magharibi na vyama visivyo vya kiserikali  kuwa waangalizi wa uchaguzi.

Wapiga kura wataamua Jumamosi ikiwa watapitisha katiba mpya ambayo inajumuisha rais kutawala mihula miwili ya miaka mitano.

Kiongozi wa kiimla wa Zimbabwe  Robert Mugabe ameshikilia madaraka tangu mwaka 1980 kwanza kama waziri mkuu na baadaye Rais. Mapendekezo hayo ya ukomo wa utawala hayatajumuisha siku za nyuma ikimaanisha kwamba Bw.Mugabe anaweza kubaki madarakani kwa miaka mingine 10.                          Habari na picha kwa hisani ni ya VOA SWAHILI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!