Je, ni lipi unajua kuhusu mapango ya Amboni?
Mapango ya Amboni yapo kilomita nane kaskazini ya mji wa Tanga, katika kijiji cha Kiomoni, kandokando ya barabara ya Mombasa.
Mapango hayo ya chokaa(limestones)yalifanyika zaidi ya miaka milioni 150 iliyopita.
Mapango yalitumika kama mahali patakatifu katika miaka 16 baada ya kuzaliwa Kristo, baada ya mtu kugundua uundaji wa maumbo mbalimbali, baadhi yao yakiwakilisha viungo vya binadamu, Bikira Maria, meli, ndege na kadhalika,
Wenyeji waishio katika eneo la mapango hutumia mapango hayo kama sehemu ya matambiko.
Mapango ya Amboni yamegawanyika katika sehemu mbalimbali.Mfano wa sehemu hizo ni kama zifuatazo,
Eneo la kwanza ni 'Mzimu' eneo ambapo watu mbalimbali huenda kwa huduma za kiibada(tambiko); eneo la pili lina tabaka tatu za majabali, ambayo wanafunzi kutumia kwa ajili ya masomo yao.
Eneo la tatu lilikuwa ni maficho ya wapigania uhuru wawili, Osale Otango,wa Mau Mau kutoka Kenya na Paulo Hamis kutoka Tanzania. Osale Otango na Paulo Hamisi waliiba mali na kuwatisha baadhi ya wakoloni katika ukanda wao na vilevile baadhi ya wenyeji walisadiki kuwa walitumia uchawi katika harakati zao hizo.
Ingawa serikali iliwachukulia Osale na Paulo kama wahalifu, wananchi waliwachukulia katika harakati za kudai uhuru, waliwachukulia kama wapigania uhuru.
Baadhi ya vivutio vilivyoko katika mapango hayo ni popo ambao hutoka nje ya mapango wakati jua linapozama. Vilevile kuna miamba yenye maumbo ya sofa, meli, mamba,tembo, ramani ya afrika, kichwa cha simba wa kiume na statue of Liberty.
No comments:
Post a Comment