Saturday 23 March 2013

CUF. YATAKA WACHINA WASIJE NA WAFANYAKAZI WAO- WATANZANIA WANAWEZA KUFANYA SHUGHULI HIZO.


Mh. Ibrahim Lipumba. mwenyekiti wa Cuf.


Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.

Serikali iwe makini na kuhakikisha hatuleti Wawekezaji matapeli kama muwekezaji wa Ujenzi wa Terminal ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Ulinzi wa mazingira uzingatiwe katika uwekezaji wa viwandani... na katika uvunaji wa maliasili yakiwemo madini.

TUMKARIBISHE KWA SHANGWE NA VIFIJO RAIS XI JINPING LAKINI TUWE NA MIPANGO MADHUBUTI ILI TUNUFAIKE NA USHIRIKIANO NA CHINA
Katika nchi nyingi za kiafrika kuna manun’guniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika. Makampuni ya China yanawekeza katika nchi za kiafrika hasa katika sekta ya madini na yanashiriki katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara. Wafanya biashara ndogo ndogo toka China wamejitokeza katika nchi nyingi na kuzua mjadala kuwa wanachukua fursa zinazopaswa kuachiwa Waafrika wenyewe.
Tanzania inaweza kutumia fursa zilizopo katika kuwa nyuma katika maendeleo ya uchumi na teknolojia. Ikiwa tutajipanga na kutumia teknolojia iliyopo tunaweza kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji kama walivyofanya Wachina. Mfumo wa soko unaofanya kazi kwa ufanisi ni sharti muhimu la kuchochea ukuaji wa uchumi unaoongeza ajira. Bei ya bidhaa na mishahara ya nguvu kazi iambatane na upatikanaji wake.










No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!