Thursday, 25 November 2021

MADHARA MAKUU 04 YA UGONJWA WA KISUKARI

1. KUFA KWA MACHO

Huwezi Kusoma,Huwezi Kuona uzuri wa mkeo kwa macho, Hutaona Mali ulizokuwa unazitafuta. Yaani (Magari,Pesa na majumba) vyote hutaviona kwa macho vizuri. Labda Upate msimamizi wa Kuviangalia hivyo.
.
2. HISIA ZA MAPENZI HUPOTEA KABISA
Utashiriki kwa Taabu na usiweze kabisa Maisha yako Yote. Ugonjwa wa Kisukari Unaongeza Hasira Jaziba Mawazo na Kukosa Furaha kabisa ya maisha. Kiasi kwamba kama Mwanamke bado Yuko vizuri na mwanaume Nguvu za Kiume zimeisha hata kama Mwanamke Hatoki nje ya ndoa "Mwanaume huwa ana wivu mkali na ugomvi kila siku kwa kuhofia mke wake anatafuta mapenzi nje ya ndoa". Jambo hili ni zito sana Usiombe Likukute kwenye Familia yako. Mwanamke unakuwa na Msongo na Hasira na bado mwanaume naye anakuwa kwenye hio hio hali. Kinga ni Bora kuliko Tiba.
3. KUFA KWA OGANI MOYO FIGO NA UBONGO
Utegemezi wa Dawa na maumivu Maisha. Ugonjwa wa Kisukari Usipodhibitika vizuri huleta Ulemavu wa Kudumu kwenye Ubongo (Kiharusi), Kwenye Figo (Figo kufa), Kwenye Moyo (Moyo kutanuka) na Mishipa ya damu kuchakaa.
Haya Yote yatakufanya kuwa Tegemezi wa dawa milele na Kibaya zaidi mapito ya maumivu ya mwili yasiyokoma maisha yote uliyobakiza duniani.
.
Wengi huwa hawapendi dawa za Hospitali lakini usipojali afya yako dawa hizo hazikwepeki maana ndio namna pekee ya kukunusuru uhai wako ukiwa katika hali mbaya. Jali afya yako linda afya yako kabla hujaitwa mgonjwa.
.
Ugonjwa wa Kisukari huchukua miaka mingi kujitengeneza madhara yake huanza kabla hata haujajitokeza. Huchukua takribani miaka 5-10 ugonjwa wa Kisukari kujitengeneza kabla haujaibuka (Kugundulika) ila madhara yake huanza mapema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!