Jinsi ya Kutunza Kitovu cha Mtoto Kama mtoto amezaliwa hospitali ambako huwa wanazingatia usafi wa hali ya juu wakati wa kukata kitovu haujitaji kuwa una futa kitovu kwa spirit au kwa iodine.
Pia unaweza kukunja nepi na kuacha kitovu wazi. Muoshe mtoto kwa kumfuta na kitambaa, usimmwagie maji. Acha kitovu kikauke chenyewe kinawahi zaidi kudondoka. Kwa kawaida, kitovu huwa kinadondoka ndani ya siku 7 na kwa baadhi ya watoto kitovu kinaweza kuchukua hata wiki 3 kudondoka. Iwapo baada ya wiki 3 kitovu hakijatatika hiyo sio hali ya kawaida nenda hospitali
No comments:
Post a Comment