Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, jijini Dar es Salaam limethibitishwa na Jeshi la Polisi huku likisema wanaendelea na msako wa kuwabaini walipo mahabusu hao.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Jumanne Murilo alipotafutwa na Mwananchi azungumzie tukio hilo, alisema yuko msibani Kibondo, atafutwe kaimu wake, Daniel Shila ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda ya Maalum Dar es Salaam azungumzie hilo.
Kamanda Shila alipotafutwa na Mwananchi alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema “waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo, si wale wenye kesi mbalimbali.”
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment