Hukupa mwongozo
Awali ya yote, malengo hukupa mwongozo na mwelekeo maishani mwako. Malengo hukuwezesha kubaini kitu unachokilenga, na hukufanya uelekeze nguvu zako kwenye kitu husika.Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na yule, malengo yatakuwezesha kufahamu unatakiwa kufanya nini au kuwa nani.
2. Hukuwezesha kufanya maamuzi
Baada ya kujiwekea malengo utaweza kubaini ni maamuzi gani yanafaa na ni yapi hayafai kulingana na malengo uliyojiwekea.
Pia utaweza kufahamu mambo ya msingi maishani mwako, hivyo utaweza kufanya maamuzi kulingana na mambo hayo.
Mtu mwenye malengo huwa makini kwenye maamuzi yake kwani analinda asije akafanya maamuzi yatakayoathiri lengo lake.
3. Hukuwezesha kutawala baadaye yako
Unapokuwa na malengo na mipango stahiki ya kuyatimiza, ni wazi kuwa moja kwa moja umeshatawala baadaye yako.
Kuweka malengo ni jambo zuri ambalo litakuwezesha kufahamu aina na mfumo wa maisha yako ya baadaye. Jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa unaweka mipango sahihi na inayotekelezeka ya kutimiza malengo yako.
Ni muhimu kuhakikisha kila siku kuna kitu kinachofanyika ili kukamilisha sehemu fulani ya malengo uliyojiwekea maishani.
No comments:
Post a Comment