Friday, 27 August 2021

Mbaroni kwa kubaka mwanafunzi wa miaka 10


Malick Apolonary mwenye umri wa miaka 20 anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Tanga baada ya kukutwa akifanya tendo la ndoa na mwanafunzi wa miaka 10 anayesoma darasa la nne katika shule ya msingi Chanika.

Akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Handenj Siriel Mchembe, ameagiza kuchukuliwa hatua kali na za haraka ili kutoa mfano kwa wengine wenye tabia kama hizo
“Tukio la kijana Malick aliyekutwa akimbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10, ni tukio la wazi, ushahidi upo na amekamatwa eneo la tukio. Jambo hili limeniumiza kama mama na kama Mkuu wa Wilaya, na hata Rais Samia Suluhu jambo hili litamuumiza pia” amesema DC Mchembe

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!