Friday, 27 August 2021

AINA ZA SELI HIZI UKIZIONGEZA UNADHIBITI KISUKARI MILELE

 
Hapa duniani Kuna matibabu aina mbili ya Kisukari, Matibabu ya Kumfundisha Mgonjwa jinsi ya kuishi na Kisukari milele (Diabetic Care Treatments) na Matibabu ya Kuondokana na Kisukari (Diabetic Remission Treatments). Vyuoni duniani Kada zote za afya huwa mitaala Yetu Tunafundishwa "DIABETIC CARE TREATMENTS na Sio DIABETIC REMISSION TREATMENTS. Kwa hio Ili Uweze Kujifunza Mbinu za Kutokomeza Kisukari mwilini HUTEGEMEA NA JUHUDI BINAFSI ZA KUJISOMEA NJE YA MTAALA HATA WA U-PROFESA.


Sayansi Inasema, Unapokuwa Huna kisukari Seli zako zinakua zinapokea maelekezo haraka ya kutumia sukari kutoka kwa mratibu Insulin. Hali hio huitwa Insulin sensitivity ya seli ni nzuri.
.
Kadri Umri unavyo enda inategemea na maisha uliyochagua kuishi na Ukoo wenu kama unadhurika na vyakula kwa wepesi. Seli zako zinaanza Kudumaa na Kuchakaa Ule uharaka wa Kupokea maelekezk ya kutumia sukari kutoka kwa Homoni inayo ratibu matumizi ya sukari "Uharaka Unashuka na Uwezo wa seli Kupokea sukari Unazidi Kupotea siku hadi Siku mpaka Unaitwa Mgonjwa wa Kisukari". Kitalamu tunasema seli zako za mwili zimekuwa Insulin resistant.
.
Ugonjwa wa Kisukari aina ya pili Ni ugonjwa wa Uchakavu wa mwili unapotaka kuukabili Usifikirie ni Ugonjwa wa Hitilafu wa Seli moja au Kiungo Kimoja. NI HITILAFU YA ASILIMIA KUBWA YA SELI ZA MWILI na MWILI MZIMA UNATAKIWA MATENGENEZO.
.
Ina maana Usipobadilisha Matendo Yaliyo fubaisha seli zako na Ukaugua Kisukari Hutakuja Kuondokana na Kisukari. Wengine Huwa Wanajistukia na Kujirekebisha kidogo (Hawaachi matendo hayo kabisa). Ndio utapata nafuu lakini Ugonjwa Utaendelea Kujisuka ingawaje makali yatapungua ila mbeleni UTAKUJA KULIPUKA KWA KASI YA 5G.
.
Wengi hampendi ushauri wangu lakini wachache wanaoweza wana furahia matunda ya Programu yangu. Huwezi ukala chakula Kilicho dhuru mwili kwa uchache ukitegemea mwili hauta endelea Kufubaa.
.
Haya huongeza Idadi ya seli zinazogomea Sukari. Na kuukuza Ugonjwa wa Kisukari.
1. Matumizi ya Wanga na Sukari. Si vizuri kula kitu ambacho mwili hauwezi kutumia hata kwa Uchache. Ushauri wa "Kula Ngumi ya Ugali, Ngumi ya Wali, Matunda matamu" Huangamiza na Kufubaza mwili kila kukicha.
2. Ini la Mgonjwa Wa Kisukari Lisipodhibitiwa Kutema Sukari. Hasa wale ambao wamegomea dawa za Kisukari
4. Pombe na Sigara na Starehe Zinginezo
5. Kukosa Mazoezi ya Viungo
6. Mafuta yenye Free radicals nyingi na Omega 6. Mafuta ya Mgando na Kimiminika yatokanayo na Mbegu za Mimea.
7. Kukosa Usingizi wa Kutosha
8. Msongo wa mawazo
Mambo hayo sita huongeza Asilimia ya seli ambazo ni Insulin resistant na Hupunguza idadi ya seli ambazo ni Insulin sensitive. Ina maana Unaongeza Usugu wa Kisukari Kila Kukicha na Kudhoofisha mwili Kinga na Matumaini ya Kuishi ukiwa na amani ya mwili Yanapotea.
.
Mambo Haya Yanafanyia matengenezo mwili na Kupunguza idadi ya seli ambazo zimegomea sukari Insulin resistant cells na Kuongeza Idadi ya seli nzima Insulin sensitive cells.
1. Kuacha kula Vitu ambavyo mwili hauwezi Kutumia. Sukari na Wanga. Fuata Programu ya Kitabu cha Sayansi Ya Mapishi.
2. Acha Kabisa Pombe Sigara na Hanasa zozote za Vilevi
3. Fanya mazoezi angalau kila siku ambayo mwili Unayamudu.
4. Jitahidi Kuzuia Ini ili lisiteme Sukari hasa wakati usugu wa Kisukari bado ni Mkubwa. Wasiliana na Daktari anaye kusimamia. Hili huwa tunafanya kwa Wateja wetu wote.
5. Pikia mafuta Imara kwenye moto na yanayo Poza mwili. Mafuta ya Nazi, Mafuta yatokanayo na Maziwa nyama, mafuta ya mzeituni (Zingatia matumizi yake Kwenye Kitabu kwa usahihi zaidi) nk
6. Tibu mwili upoe, Upate usingizi wa kutosha na Jifunze Namna ya kuepuka msongo.
.
NB:
Je Unahitaji Kupunguza Uzito na Kitambi? Tuna Kozi Maalumu kwa wanaopenda Kusimamiwa na Clinic yetu popote walipo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!