Sunday, 18 July 2021

TUKIO LA MAUAJI SINZA AMPIGA RISASI MWENZAKE NA KISHA KUJIUA/ALITISHIA KUUA WENGINE

Katika Bar ya Lemax huko Sinza kwa Remmy mtu mmoja amedaiwa kuwatishia wenzake bastola ambapo baadaye alimpiga kijana mmoja risasi tatu (Kichwani, tumboni na pajani) na yeye mwenyewe kujipiga


Wengi wetu tumeona video na picha zilizosambaa za tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.

Kwa mujibu wa shuhuda ambae pia ni Rafiki, Kijana aliyepigwa risasi na kufariki anaitwa Gift na alikua amekaa jirani na Alex na alisimama kumtuliza Alex baada ya kuona ameanza kutishia Watu kwa bastola yake, amesema Shuhuda huyu.
“Gift ni Kijana mwenzangu tukifanya kazi Ofisi moja, alikua ana muomba Alex asipige risasi kama vile na kupoteza amani, yani kitendo cha Gift kumsemesha yule Jamaa imekua kama kosa aligeuka akammiminia Gift risasi nyingi kama mbuzi, Gift kuona vile akakimbia lakini akaishiwa nguvu hatua chache tu”
“Tulishindwa kutoa msaada kwa Gift kwasababu Jamaa mwenye Bastola (Alex) alikua kama amevurugwa Shetani kama amemuingia anageuka anaangalia nani mwingine ampige risasi…………..”





No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!