Mwanamke mmoja mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuchoma moto nyumba ya mpenzi wake aliyetambulika kwa jina moja tu la Kelvin.
Dada huyo (Tina) amefanya tukio hilo leo huku wivu wa kimapenzi ukitajwa kusababisha hasara hiyo kubwa.
Mwanaume huyo hakuwa ndani wakati mpenzi wake huyo akiichoma nyumba hiyo hivyo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha kwenye kisa hicho.
Tukio hilo linatokea ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu ugomvi kama huo usababishe kifo cha mwanaume mmoja aliyefungiwa ndani ya nyumba na kisha kuteketezwa kwa moto na aliyekuwa mpenzi wa mwanaume huyo.
No comments:
Post a Comment