Tuesday, 25 May 2021

Walioua Mikocheni?

Polisi Kanda Maalum ya DSM inawashikilia Watu watano ambao ni Issa Karim maarufu Mdaka Bomu (33) wa Mbezi, Mohamed Juma maarufu (Miaka 31) wa Mbezi Mwisho, Selemani Seif maarufu Dullah Kishandu (34) wa Mbezi Mwisho, Samsoni Joseph maarufu Mjeuri (32) wa Mbezi na Ezekiel Kennedy maarufu Simba MC wa Mbezi kwa tuhuma za mauaji.


“May 08, 2021 majira ya mbili usiku Mikocheni A Watuhumiwa walivamia Bar iitwayo Imbizo na kumshambulia kwa mapanga na marungu Mlinzi (Regan Sylivester) na kusababisha kufariki dunia papo hapo, pia wanatuhumiwa kuhusika na tukio la unyan’ganyi wa kutumia silaha huko Mabwepande May 07, 2021 saa tatu usiku walipovamia Petrol station ya MEXONS na kuwashambulia Walinzi, Wahudumu na Wateja na kupora Tsh 2,440,000/= na kisha kupora silaha ya Walinzi aina ya short gun” Polisi DSM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!