Tuesday, 25 May 2021

MAMBO KUMI LABDA HUYAJUI KUHUSU KITAMBI NA UZITO MKUBWA

 


1. Seli za Mwili huwa zinapenda Kuchoma Sukari kama chaguo la Kwanza la Kuupa mwili nishati hata kama umekula vyakula vya mafuta na Protini. Seli huwa zina mahaba sana na Sukari /Vyakula vya wanga.

2. Mwili Unapokua Unachoma sukari Huwa hauwezi Kuchoma mafuta. Hivyo basi mafuta huchomwa baada ya wanga uliyokula kuisha na hazina ya sukari glycogen kuisha mwilini. Hivyo Inachukua muda mrefu sana zaidi ya masaa 12 mwili kuanza kuchoma mafuta kama Chakula chako Unaambatanisha na wanga. Ni ngumu kuunguza mafuta kama ilivyovigumu kupata hela ya Benki kama mwili unachoma Sukari.
3. Mwili Unapokua Unachoma Sukari Unakuwa Masika yaani Mazingira ya uhifadhi na mwili ukiwa unachoma mafuta unakuwa katika mazingira ya kupunguza hazina "Unachoma mafuta ya ziada"
4. Ukitaka seli za mwili Zichome mafuta moja kwa moja kama chanzo cha Nishati ya mwili. Punguza kiwango cha sukari na wanga katika sahani. Ili seli za mwili zitakapokosa wanga zikimbilie kuchoma mafuta
5. Njia ya pili ni Kudhibiti Idadi ya milo. Milo inapokua mingi hata kama unakula vyakula vya programu ya sayansi ya mapishi bado huwezi Kupungua. Kila unapokula Homoni zinazoshikilia na kuzuia mafuta hupanda matokeo yake hutapungua vizuri. Hivyo Jitahidi kudhibiti idadi ya milo au Kufunga mara kwa mara yaani "Mfungo Tiba"
6. Mwili unapokua unachoma Sukari huwa haupo kwenye matengenezo lakini mwili ukiwa unachoma mafuta unakuwa kwenye matengenezo.
7. Mwili unapokua unachoma sukari huzalisha vileta majeruhi katika viungo vya mwili vingi yaani Free radicals nyingi ambazo huvimbisha na kufubaza mwili endapo mwili ukizidiwa uwezo wa kuondoa kwa kutumia Ant Oxidants. Lakini mwili unapokua unachoma mafuta huzalisha vipoza mwili Ant Oxidants (BHB) ambazo husaidia Kutibu Asthma,Degedege,Kansa,Kisukari,Presha nk
8. Duniani Kote Wapishi wote wanafahamu Vitoweo ni Vyakula vikuu katika sahani na Wali ndizi viazi ni vyakusindikiza mlo mkuu. Unapolipia hela Hotelini huwa tunalipia "Pesa ya Kitoweo vilivyo ambatanishwa huwa ni Bure". Kwa mama ntilie na Majumbani Tumepiga sarakasi "Nafaka na Wanga Mizizi Tumevifanya kuwa mlo mkuu kwa sababu ya mwongozo wa Lishe (SAD) mwaka 1977 MWONGOZO ULIOUNDWA NA RAIS WA AMERIKA RICHARD NIXON.
9. Zamani tulikaririshwa kwamba chakula chenye Kalori nyingi kama mafuta hunenepesha kuliko vyakula vyenye kalori kidogo kama wanga ambavyo hadi sasa vinasemekana havinenepeshi kwa sababu havina mafuta. Ukweli ni kwamba Mafuta yaliyohifadhiwa mwilini kwa asilimia 95 yanatokana na sukari iliyokosa kwenda kutumika hivyo hubadilishwa kuwa mafuta kama hazina ya matumizi ya baadae. Kitambi kinatokea pale hazina hii ya sukari inapokua inaongezeka Kila siku. Kitambi kwa mujibu wa homoni sio ulafi na sio uvivu ni matokeo ya homoni zinazohifadhi mafuta kufanya kazi katika kiwango cha juu kwa sababu ya machaguo mabaya ya vyakula hasa vyenye sukari nyingi. Hakuna mtu ambaye anaweza kunenepa kwa kumpa Vyakula vya Mafuta.
10. Elimu ya Kalori na Elimu ya Cholesterol au Lehemu Imeangamiza watu wengi sana. Mfano Tunaacha kula vyakula asili tunakimbilia vyakula vya Kuundwa na mkono wa binadamu. Maziwa asili yenye mafuta unaacha unachukua ambayo hayana mafuta eti kwa sababu yamechujwa mafuta. Maziwa asili unaacha unakimbilia maziwa ya Unga. Unaacha kula yai zima na kiini chake unatupa kiini unakula Jeupe tu. Nyama unayochinja ni mbaya mpaka ikienda kiwandani ikamuliwe mafuta ndio iitwe nzuri. Mafuta ya mgando asilia kama Samli siagi Nazi ambayo yanatumia teknolojia ya sufuria na moto Elimu hii iliyapinga na kuyapiga vita. Elimu hii na Mwongozo huu wa chakula umetufanya Tubadilishiwe Vyakula kwa sababu ya mapinduzi ya viwanda. Hivyo basi hatuna budi kuishi na magonjwa yatokanayo na mapinduzi ya Viwanda. Sayansi ya mapishi Inakufundisha Kurudia Vyakula Asilia ambavyo Babu na Bibi zetu Walikula na Waliishi na afya njema.
.
Kama Umejifunza Utajifunza zaidi katika KITABU CHA MWONGOZO WA LISHE SAYANSI YA MAPISHI
Kama Unataka NAKALA YAKO tuma sms Kwenda 0787999994 au 0767 074 124

Dr. Boaz Mkumbo MD

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!