Monday 1 March 2021

Watu 66 wapoteza maisha kutokana na virusi vya Corona (Covid-19) ndani ya saa 24 nchini Uturuki

Watu 66 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya Corona (Covid-19) ndani ya saa 24 nchini Uturuki.

Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya Corona tangu kuzuka kwa janga hilo hadi kufikia sasa nchini Uturuki ni 28,569.

Jumla ya watu 109,639 waliweza kufanyiwa vipimo vya covid-19 ndani ya siku moja ambapo kesi 610 ziligundulika, idadi ya maambukizi ndani ya siku moja imefikia 8,424.

Idadi ya waliopona imefikia 2,572,234 ikiwa ni pamoja na watu 6,511 walioruhusiwa kuondoka hospitali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!