Ndugu watano wa Familia moja waliofariki kutokana na msongamano mkubwa uliotokea wakati wa kumuaga Hayati Dr. John Pombe Magufuli Uwanja wa Uhuru, wamezikwa jana kwa pamoja kwenye makaburi ya Familia yao yaliyopo nyumbani kwao Kimara Mwisho Dar es salaam.
Ndugu hao ni Suzan Mtuwa pamoja na Watoto wanne ambao aliongozana nao wakiwemo Watoto wake wawili aliozaa na Mumewe Denis Mtuwa ambao ni Natalia na Nathaniel, pia Watoto wawili wa Kaka zake Denis ambao ni Chris na Michelle.
Kwenye tukio hilo Suzan aliongozana pia na Dada wa Kazi aitwaye Anitha ambaye na yeye pia amefariki Dunia na taratibu za mazishi yake zinaendelea.
Kwa sasa Denis Mtuwa amempoteza Mkewe Suzan na Watoto wake wawili (Natalia na Nathaniel) na sasa amebaki na Mtoto mmoja mdogo ambaye siku ya tukio hakwenda Uwanjani.
#RIPNduguZetu
No comments:
Post a Comment