Saturday 6 March 2021

Mume na Mke wafariki baada ya gari walilokuwa wanasafiria kusombwa na maji

 


Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Kanda ya Kati Dr. Haruna Chawala na Mkewe Neema Mwasanganga wamefariki baada ya gari walilokuwa wanasafiria kusombwa na maji eneo la daraja la Shaaban Robert Mpwapwa, Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti Tanzania Dr. Jonas Kizima amethibitisha na kusema Dr. Chawala alikuwa anampeleka Mkewe kazini kwenye Hospitali ya Wilaya lakini walipofika kwenye daraja hilo maji yaliwazidi na kusombwa jana saa mbili usiku.
Mashuhuda wanasema mwili wa Mkewe ulikutwa kitongoji cha Kwamshango kilometa 15 kutoka walipotumbukia wakati mwili wa Dr. Chawala ulikutwa kitongoji cha Isinghu umbali wa kilometa 18, miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mpwapwa ikisubiri taratibu za Ndugu na Serikali. #RIPNduguzetu 🙏🏿

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!