Saturday, 20 February 2021

Zamaradi Mketema -''Kama hawataki upite kwenye njia yao.. tengeneza ya kwako!!

 


''Kama hawataki upite kwenye njia yao.. tengeneza ya kwako!! Najua sio rahisi na huenda hujui unaanzia wapi, ukiangalia mbele ni msitu, vigingi na majani marefu ambayo huoni kama kunawezekana.. Lakini hata wao haikuwa rahisi pia!! Ila KULIWEZEKANA..

We unashindwaje!!? kitu kimoja pekee kitakufanikishia.. NIA YA KWELI!! Ingia mzigoni kwa moyo wote, Fyeka inapobidi, Angusha miti, kata magugu.. Itatokea tu!!! Na ukifanikiwa utapita bila bugudha za wengine kwa Raha na UHURU!! Sababu ni wewe ulietoa jasho.. na zaidi utakuwa na mamlaka na sauti juu ya hiyo ya Kwako pia, kikubwa achia wengine wapite!!! Ni Njia tu.. tena kupita kwa wengi ndio kutafanya iendelee kuwa SAFI na sifa yake ienee tofauti na isiyopitika/kutumika, majani yatarudi na itapoteza sifa yake!! Na zaidi hatutaitambua tena kama Njia!! '' @zamaradimketema

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!