Thursday, 18 February 2021

UPUNGUFU WA MADINI YA ZINC NA MADHARA YAKE MWILINI.

 Zinc ni elementi muhimu mno katika afya ya binadamu hivi kwamba ukosefu kidogo unaweza kuleta madhara makubwa. Zinc ni ya muhimu sana kwa sababu inapatikana ndani ya kila kiungo cha mwili cha binadmu na inahusika kwa karibu sana na kugawanyika kwa seli za mwili. Ni antioxidant yenye nguvu sana, inayosaidia kuzuia kansa, na pia inahusika moja kwa moja katika ufanyaji kazi wa tezi mbalimbali za kutengeneza homoni na kuweka sawa viwango vya homoni katika mwili. Inaonesha kuwa asilimia kubwa ya watu duniani wanakabiliwa na upungufu wa zinc na kwa sababu mwili wa binadamu hauhifadhi zinc, tunalazimika kupata zinc kila siku.


VYANZO VYA MADINI YA ZINC
Kwa msomaji wa makala hii, tambua kwamba huhutaji kwenda mbali zaidi kupata madini haya muhimu kwa afya yako, maana hupatikana kwenye vyalula vinavyotuzunguka kiurahisi kama
1.maini
2. mboga za spinach
3. mbegu za maboga na karanga
4. nyama nyekundu
5. maharage na maziwa na
6. Uyoga na Parachichi
Baadhi ya dalili ambazo zitakusaidia kutambua kuwa una upungufu wa madini ya zinc ni pamoja na
Ø Kupoteza hamu ya kula
Ø Kujiskia vibaya na huna mood mara kwa mara
Ø Kupungua kwa uwezo wa kutambua ladha ama harufu ya kitu
MADINI YA ZINC HUSAIDIA
1) Kusawazisha kiwango cha sukari katika mwili
2) Kusaidia utengenezwaji wa protini kwenye mwili
3) Kusaidia kusapoti mfumo wa upumuaji
4) Kuongeza ufanyaji kazi wa seli za mwili
5) Kupunguza sumu mwilini na kusaidia mmengeyo wa chakula
UPUNGUFU ZA ZINC NA AFYA YA UZAZI
Upungufu wa zinc husababisha ugumba kwa jinsia zote, wanaume na wanawake na kuwasababishia tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango kidogo cha zinc katika mwili hukuza madhara ya msongo wa mawazo katika mwili na kuchochea uzeekaji wa haraka. Isije ikafikiriwa kuwa upungufu wa zinc upo zaidi kwa watu wenye lishe duni au wale katika nchi zinaendelea tu. Ukweli ni kuwa tatizo hili lipo kila mahali duniani na kwa wanaume, wanawake na watoto.
Upungufu wa zinc hubadili namna ya kusikia ladha na kusababisha kupenda chumvi zaidi, chakula kitamu zaidi. Inaweza kujidhihirisha kwa kuharisha, upungufu wa nguvu za mwili, uchovu sugu, ugumba, upungufu wa kinga za mwili, kukosa kumbukumbu, kushindwa kutuliza mawazo, kuchelewa kupona vidonda, neva kutofanya kazi vizuri, na kuunguruma kwa sauti kwenye masikio.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanamme:
Zinc ni madini ya lazima katika kuweka testosterone kwenye kiwango kinachotakiwa, na seli za tezi dume ya mwanamme zinahitaji kiwango cha zinc ambacho ni mara 10 zaidi ya mahitaji ya seli nyingine za mwili ili ziwe na afya na zifanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Upungufu wa zinc kwa wanaume huathiri uzalishaji wa testosterone, huwaweka wanaume kwenye mazingira hatarishi ya kupata saratani ya tezi dume, na huwasababishia ugumba. Upungufu wa zinc umehusishwa na kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanamke:
Kwa wanawake, zinc inahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!