Monday, 22 February 2021

Je ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NI AFYA?

Jibu ni H A P A N A. Inatakiwa Ule Matunda kwa AKILI au Utaratibu.

Kwenye Matunda Tunapata Viini Lishe kama Sukari (Fructose na Glukosi), Vitamin na Madini. sasa Kila kiini Lishe Unachopata kwenye Matunda Kina Usahihi wake na Utaratibu wake Endapo Ukirejea Sayansi ya Kitabu cha Mwongozo wa Lishe SAYANSI YA MAPISHI.


1. KIWANGO CHA FRUCTOSE NA GLUCOSE NA USTAHIMILIVU WA MWILI.
Kila binadamu ana Ustahimilivu wake wa Sukari ili awe na afya njema. Hivyo KIWANGO cha Matunda hasa Yenye SUKARI NYINGI (Yale Matamu) hutofautiana Mtu na Mtu. Huwezi Ukatoa Ushauri wa UJUMLA kwamba WOTE MLE MATUNDA KWA WINGI NA MTASEMEKANA MNAZINGATIA LISHE BORA.
.
Makundi ambayo yanatakiwa Yapata ushauri maalumu ya Ulaji wa matunda hasa matamu ni Wenye Uzito mkubwa na Kitambi, Watarajiwa wa Kisukari na Wenye Kisukari Rasmi, Wazee na Watoto.
.
Fikra ya Ulaji wa matunda mengi ni afya Ina angamiza wengi sana unatakiwa ule kulingana na HALI YAKO KIAFYA ILIVYO SASA.
.
Mfano: Mtu ana Uzito Mkubwa anapokula matunda kwa wingi Tikiti au Nanasi Lote anamaliza au Anakamua juisi ya Embe au Nanasi. Vitendo hivi Vitamuuza Huyu. Kwanza Uzito utaongezeka kwa Spidi sana, Pili kwa Unene wake hajijui yuko hatua gani za Ugonjwa wa Kisukari. Ina maana Atakuwa anachochea matatizo yake yajitengeneze zaidi.
.
Mbali na Sukari (Fructose na Glucose) Kwenye matunda Huwa tunapata Vitamins. Na aina ya Vitamin ambazo Hupatikana Kwenye matunda kwa wingi ni Water soluble Vitamins (Vitamin C na B Vitamins). Maana ya water soluble ni Kwamba kundi hili la vitamin Hutembea na Maji. Pia Mwili wa Binadamu Huwa kisayansi Inajulikana kwamba Hauna Mfumo wa Kuhifadhi WATER SOLUBLE VITAMIN ENDAPO Ukizidisha au Ukizila kwa wingi Kuliko matumizi ya mwili.
.
Mfano: Wewe Ukajenga Tabia Mbaya ya Kukamua Juisi ya Maembe Mananasi Papai ndizi Miwa unywe kwa malengo ya kupata Vitamin Nyingi. Nakukumbusha tu ni kwamba Mwili utavuna Vitamin Ambazo unahitaji kwa matumizi yake ya siku. Kiwango chochote kilicho Pitiliza mahitaji ya mwili Kitatolewa mwilini kwa Njia ya mkojo. Mwili huwa hauhifadhi Water soluble vitamin na Hauna huo mfumo, Hivyo ukizidisha mwili huziachia zitoke kwenye Mkojo.
.
.
Je Baada ya mwili Kuvuna Vitamin zinazotembea na Maji na Zote zilizozidi Zikatolewa nje kwa njia ya mkojo. Je sukari huenda wapi?
Jibu: Sukari (Fructose na Glucose) Hubakia Mwilini. Kwani mwili wa binadamu huwa Haukubali kupoteza Nishati ya Sukari Kupitia Figo. Ndio maana Ukiona Kwenye Mkojo kuna Glucose huwa sio ishara njema kitalamu. Kwa maana hio Ile Sukari Uliyo mimina Mwilini yote Itaenda Kubaki mwilini kama Hazina yaani MAFUTA na GLYCOGEN. Ina maana Unywaji wa Juisi za matunda matamu Unaumiza Mwili wako kwa Kuendelea Kukunenepesha, Kufubaisha mwili wako, na Unaweza Kuibua kisukari Presha na maradhi mengine ya lishe yaliyokuwa yamejificha mwilini.
"Kiufupi mwili huwa haujui Kutofautisha hii ni Sukari ya soda na Hii ni Sukari ya Juisi ya Miwa au Embe au Nanazi na Mchakato wake mwilini Unapitia hatua zilezile"
.
Usipumbazike Kwamba kuna "Sukari Asili" na "Sukari ya Kiwandani" Kumbuka "Glucose ni Glucose" pia "Fructose ni Fructose". Kitendo Jamii Ilicho Kosea ni Kupokea mafundisho Angamizi kwamba Badala ya Soda Unywe Juisi asili au Mlima wa matunda Asili.
.
Tumeona Mwili Hauna mahitaji makubwa ya water soluble vitamin na hata ukiupendelea kwa kuunywesha Juisi Utazikojoa Vitamin zote ambazo zimezidi kiwango cha matumizi ya mwili kwani Mwili hauna mfumo wa Kuhifadhi vitamin hizo zinazotembea na Maji mfano Vitamin C na B Vitamins isipokuwa B12.
.
Kadri Unavyo Mimina Juisi na Sukari kutoka kwenye ulaji wa holela wa matunda Unaongeza Hazina Ya Mafuta mwilini kwenye Ini Figo Moyo na Chini ya ngozi yanayo Tengeneza Nyama Uzembe.
.
Ushauri wangu Kwa Jamii Kuhusu Matumizi Sahihi ya Matunda
Jitahidi Kwanza Uwe na Mazoea Ya Kupima Afya. Fanya Vipimo Vikubwa na Vidogo. Watu tunaposema Kupima Wanafikiri ni Mkojo, Choo Malaria na HIV. Pima vipimo ambavyo vinaweza Kukugundua hata kama wewe ni Mtarajiwa wa Kisukari Presha nk Ili Ujikinge Usipate maradhi hayo. Unakutana na mtu ana Kilo nyingi hasa mpaka huruma lakini Anajimiminia juisi za matunda Asubuhi mchana na Jioni akijipumbaza ni Asilia halafu Akija Kugundulika na Kisukari anasema Kisukari hiki kimenistukiza. Ugonjwa wa Kisukari huwa haushtukizi inachukua miaka takribani 10 au chini ya hapo kujitengeneza hivyo Hizo juisi ni kama zinaibua ugonjwa ambao Ulikuwepo unajisuka kwa ndani. Badala ya kuibuka Siku zijazo kisukari kinaibuka haraka kwa sababu ya Ulaji wako wa Kutojua. Ndio maana nakushauri Ujipime kwanza Ndio utambue Mpangilio sahihi wa chakula ni upi? Daktari atakupa Mwongozo kulingana na majibu yako.
Kama Una Uzito Mkubwa, Kitambi, Kisukari, Presha inakunyemelea makundi haya yote nakushauri Upunguze ulaji wa matunda matamu na Uache kabisa Matumizi mabaya ya sukari kwenye matunda kwa Kitendo cha kukamua matunda kuwa Juisi.
Matunda usiyale Kwa kuyatengea Muda wake maalumu. Unakumbuka ule usemi Unatakiwa ule kwanza Chakula ukae Nusu saa mpka saa ndio ule matunda. Kauli hizi zitakufanya Utumie matunda Vibaya. Maana yake unataka kufanya matunda yawe ni mlo kama milo mingine mikubwa. Mimi nashauri Kuepusha matumizi makubwa ya matunda hakikisha matunda yanakuwa sehemu ya mli wako. Mwili unajua kipi kinaanza kuchukulia na kipi kitamalizia. Ukiweka matunda sehemu ya chakula chako Ukamaliza kula chakula na ukashushia matunda hapo hapo automatically Utakula kiwango kidogo sana kuliko ukikaa saa moja utakula mengi sana.
Matunda Matamu na Juisi za matunda kwa Mtarajiwa wa Kisukari (Pre diabetes) na Mgonjwa rasmi wa Kisukari Huwa Yanashusha Kinga ya mwili. Ukinywa Juisi za Matunda Huku mwili wako uwezo wa kutumia Sukari ni mdogo. Unafanya mwili uanze kuteseka kutafuta njia ya kuisafisha hio sukari. Figo huanza Kuikojoa Hio sukari unapokuwa unakojoa sana kwa lengo la Kupunguza Sukari Unapoteza Maji na Vitamin Zinazotembea na Maji (B Vitamins na Vitamin C). Ina maana Juisi za Matunda zinapunguza Kinga ya mwili kwa Baadhi ya makundi ya watu kwa sababu husababisha Upotevu wa Vitamin za Kinga ya mwili kama Vitamin C na B Vitamins. Kumshauri na Kumjengea Mtu aliyeko ktk Kundi la Utarajiwa wa kisukari na Mgonjwa wa Kisukari kwamba Tunda tamu kwa sababu ni asili halina Shida lanyewe na hata Juisi yake kwa sababu ni asilia. Unamuumiza na Unamwangamiza. Matunda kwa Mgonjwa wa Kisukari ni yale yanayolinda kinga ya mwili kwa kutoruhusu Ukojoe Vitamins sana Mfano. Parachichi Tango nk Matunda ambayo sio matamu.


KITABU KIPO MIKOA ZAIDI YA 15 TANZANIA WASILIANA NASI KWA NAMBA 0787 999 994 au 0767074124.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!