Wednesday, 11 November 2020

FREE RADICALS HULETA MAJERAHA KATIKA VIUNGO VYA MWILI NA KULETA MARADHI SUGU



Free Radicals: Hizi sumu tunazipa jina la “Reactive Oxygen species” zinaleta majeraha katika kila kiungo cha mwili ni sawa kama nimekuweka kwenye chumba chenye wadudu wengi wanaong’ata.

Hupatikana kwenye DAMU YAKO kutokana na UTENDAJI KAZI WA MWILI na KUTOKA KWENYE VYAKULA UNAVYOKULA HASA VYA KUKAANGA KWENYE MAFUTA DHAIFU.

Sumu hizi (ROS) zinahusishwa kusababisha Uzee haraka, Kisukari,Magonjwa ya moyo,Presha Pumu ya kifua,pumu ya Ngozi,Magonjwa ya kinga ya mwili kama SLE (Lupus,Vitiligo,Psoriasis), baridi yabisi (Rheumatoid arthritis) nk.
Watafiti hawa kutoka Chuo kikuu Muhimbili kitengo cha sayansi walitaka kuangalia Kiwango cha sumu hizi (Oxygen Free Radicals) kwa wagonjwa wenye Kisukari na Jinsi gani zinachangia mgonjwa wa kisukari kudhoofika kwa haraka na kupata majanga makubwa ya ugonjwa huu.
Tunapo ongelea majanga makubwa ya ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kiharusi,shambulio la moyo itokanayo na mrundikano wa mafuta mabaya kwenye kuta za mishipa ya damu,Figo kufa kabisa, viungo kuoza na kupoteza viungo, upofu nk. Sasa watafiti walikuwa wanachunguza kimaabara uhusiano wa mwili kulemewa na hizo sumu na kutokea kwa majanga hayo kwa wagonjwa wa kisukari.
Tafiti Ilifanyika kwa “Kupima kiwango cha hizi sumu kimaabara kabisa kwa wagonjwa wenye kisukari na wasiokuwa na kisukari”.

Mchango wa sumu zinazo zalishwa wakati mwili unachakata chakula na kutoka kwenye chakula ktk Kusababisha Maradhi sugu Ya Lishe.

Kwa miaka zaidi ya 4 nimewekeza Uelewa wangu wote Kama Daktari kufanya Utafiti wa marejeo Kisayansi na Machapisho mengi yanayo elezea Kuhusu Ugonjwa wa kisukari.

Tanzania tuna Upungufu mkubwa sana wa Tafiti za Kisukari hasa za Kimaabara zaidi. Ila Nimebahatika kuona Chapisho moja Ambalo limenitia hamasa kubwa sana kuona Niwafundishe Kidogo.

 

Tafiti ilifanywa na Madaktari kutoka Chuo kikuu Muhimbili walitaka kuangalia “Uhusiano kati ya mwili kuwa katika msongo wa sumu (Oxidative stress) na Kupata maafa makubwa ya kisukari kama shambulio la moyo” 2012 Dr Solomon Genet, Yakobo na Janne Lutale. (Oxidative Stress Correlates with Complications Among Diabetic Patients Attending a Diabetic Clinic in Muhimbili National Hospital, Dar es Salaam, Tanzania, 2013-4)

 

Mwili wa binadamu huwa unapata mabaki ya oxygen yaani Oxygen Reactive Species(ROS) wakati wa kuunguza chakula cha wanga,mafuta,protini nk. Endapo sumu hizi zisipo ondolewa huleta majeraha na athari kubwa mwilini.

Mwili una mfumo wa kuondoa sumu hizo ambao una endeshwa na viondoa sumu yaani Ant Oxidants kama Glutathion, Glutathion reductase,superoxide dismutase,Catalase, Vitamin D na E. Na hizo ant oxidants ndizo husafisha hizo sumu zinazo zalishwa na tunazopata kutoka katika vyanzo mbalimbali mwilini.

 

VYANZO VYA SUMU HIZI REACTIVE OXYGEN SPECIES

Hivi ni baadhi ya vyanzo kitafiti ambavyo vina hatarisha mwili kuwa katika msongo wa sumu yaani Oxidative stress na kukuhatarisha na magonjwa mbalimbali sugu yasiyo ya kuambukiza.

  1. Wakati mwili unaunguza wanga kupata nishati mwili huzalisha Oxygen Free Radicals nyingi kuliko unapo unguza chakula cha mafuta.

  2. Unapoyachoma mafuta ya Mbegu za mimea kama alizeti Pamba soya nk huzalisha sumu hizo nyingi kuliko utumiapo mafuta ya Samli,Siagi, Nazi na mengineyo ambayo sio ya mbegu za wanyama.

  3. Unapokula mafuta mgando Yatokanayo na kuchoma na kutumia kemikali kubadilisha mafuta yasiyo ganda kuwa mgando. Yaani Mafuta ya mbegu za mimea kuwa mgando mfano Margarine (Brands) zote Yanakuwa na kiwango kingi cha Oxygen Free Radicals. Mafuta ambayo tunapaka kwenye mikate,tunapikia keki ambayo ni mgando lakini chanzo chake ni mbegu za mimea yameandikwa “Vegetable Fat”

 

Sasa Endapo mwili ukizidiwa na hizi sumu, mwili unalemewa uwezo wa kusafisha hizo sumu (Reactive oxygen species), matokeo yake mwili unaingia kwenye “Msongo wa sumu”Kitalamu tunaita “Oxidative stress”

Hizi sumu tunazipa jina la “Reactive Oxygen species” zinaleta majeraha katika kila kiungo cha mwili ni sawa kama nimekuweka kwenye chumba chenye wadudu wengi wanaong’ata.

Sumu hizi (ROS) zinahusishwa kusababisha Uzee haraka, Kisukari,Magonjwa ya moyo,Presha Pumu ya kifua,pumu ya Ngozi,Magonjwa ya kinga ya mwili kama SLE (Lupus,Vitiligo,Psoriasis), baridi yabisi (Rheumatoid arthritis) nk.

 

Watafiti hawa kutoka Chuo kikuu Muhimbili kitengo cha sayansi walitaka kuangalia Kiwango cha sumu hizi (Oxygen Free Radicals) kwa wagonjwa wenye Kisukari na Jinsi gani zinachangia mgonjwa wa kisukari kudhoofika kwa haraka na kupata majanga makubwa ya ugonjwa huu.

Tunapo ongelea majanga makubwa ya ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kiharusi,shambulio la moyo itokanayo na mrundikano wa mafuta mabaya kwenye kuta za mishipa ya damu,Figo kufa kabisa, viungo kuoza na kupoteza viungo, upofu nk. Sasa watafiti walikuwa wanachunguza kimaabara uhusiano wa mwili kulemewa na hizo sumu na kutokea kwa majanga hayo kwa wagonjwa wa kisukari.

 

Tafiti Ilifanyika kwa “Kupima kiwango cha hizi sumu kimaabara kabisa kwa wagonjwa wenye kisukari na wasiokuwa na kisukari”.

 

ZINGATIA HAYA YALIYOFANYIKA KWENYE TAFITI

 

  1. Wagonjwa wenye Kisukari walikuwa 80. Ambapo Kisukari aina ya kwanza walikuwa 12 na Kisukari aina ya pili walikuwa 68.

Kingine: Katika Wale 68 aina ya kwanza wanawake walikuwa 57 sawa na asilimia 71.2. (Ukisoma kuhusu Kitambi Kisukari takwimu za wanawake huwa wanaongoza tu ufumbuzi unahitajika).

 

  1. Halafu walichukuliwa wale ambao hawakuwa na Ugonjwa wa Kisukari kabisa Kutoka Utawala wa MUHAS ili kuja kufanya ulinganifu wa majibu kiwango cha hizo sumu ROS.
  2. Walipimwa vipimo vyote vidogo vidogo BMI, Sukari,Cholesterol na Presha.
  3. Hawa wote walichukuliwa kutoka kwenye mahudhuriao ya kliniki siku hio na kupewa fomu za ushiriki wa tafiti kuweza kupata ridhaa yao (Cross sectional study-random sampling).
  4. Wote walichukuliwa sampuli za damu ujazo wa 4mls kwa madhumuni kwenda kuangalia kiwango cha Oxygen Free Radicals katika mwili wa kila anaye shiriki tafiti hio.
  5. Kimaabara walitumia teknolojia ya kutumia Dawa iitwayo Thiobarbituric Acid Solution(TBARS) ambayo ikipambana na Malondialdehyde kwenye damu hutoa rangi ya “Pinki” na kisha Kupima Ujazo kwa kutumia Spectrophotometer kwa kusoma 532nm.
  6. Majibu Wale ambao waliokuwa na kisukari katika hali mbaya zaidi ya 10mmol/L walionekana wana “Hizo sumu nyingi”Kuliko wale ambao Sukari yao walikuwa wameidhibiti vizuri. Na Wengi walio onesha kiwango kingi cha sumu walikuwa na Madhara makubwa ya Kisukari mfano kwenye moyo nk.

 

 

CHAKUJIFUNZA KATIKA TAFITI HII

  1. Watafiti wametueleza kwamba sukari nyingi kwenye damu huchangia ongezeko la uzalishaji wa sumu hizi (Reactive oxygen species). Na huchangia sana kudhooficha karibia kila kiungo ndani ya mwili wako. Pia waliona zinachangia kumhatarisha mgonjwa wa kisukari kupata shambulio la moyo kutokana na mrundikano wa lehemu kwenye kuta za mshipa wa damu wa moyo. Ina maana sumu hizi zinamuangamiza haraka mgonjwa wa kisukari kiafya.

  2. Unashauriwa Kudhibiti Sukari Yako ili kupunguza uzalishaji wa sumu hizo. Maana kadri sukari inavyo dhibitiwa una uhatarisha mwili katika kiwango kidogo sana cha sumu na mpaka hakuna. Hivyo suluhisho hapa ni kuhakikisha sukari inadhibitiwa muda wote isome katika kiwango salama.

 

PENGO KATIKA TAFITI HII ILI TAFITI ZINGINE ZINAZO FUATA ZIZIBE PENGO HILI

 

Kwanza kabisa nimefurahi teknolojia iliyotumika kiutafiti ni ya uhakika Zaidi maana ni teknolojia ya kimaabara. Kwa hio majibu haya ni ya ukweli kwa kiwango kikubwa kuliko tafiti zinazo egemea kwa wat utu kuuliza maswali basi.

Hawa watafiti wametufungulia mlango na wamemlika karabai sasa tuone nuru mpya na tujikite sasa kutafuta uhusiano uliopo kati ya msongo wa sumu na kutokea kwa magonjwa sugu ya lishe kwa taifa letu la Tanzania.

Nilipokuwa naandika kitabu changu cha nuru ya kisukari nilijikita kujadili adui mkubwa moja wapo ni mwili kuwa katika msongo wa sumu (oxidative stress) inavyoweza kukuhatarisha na ugonjwa wa kisukari. Watafiti na matibabu hayaja egemea huku wakati ni mzizi mkubwa sana unao angamiza wengi sana kiafya kimya kimya. Tuamke sasa tuongeze nguvu kuelimisha jamii namna ya kuzima moto uliosababishwa na mwili kuwa katika msongo wa sumu “Oxidative stress”.

 

Baadhi ya mapungufu yanayo hitaji tafiti Zaidi zifanyike

 

  1. Watafiti hawajasema Vyanzo Vingine Vya Sumu isipokuwa ychanzo kimoja tu walicho kijadili kwamba ni “Sukari kuwa juu sana kwa muda mrefu”kwa mgonjwa mwenye kisukari.

Tafiti zinasema kuna vyanzo Vingi kama mafuta yasiyo himili moto,matumizi ya vyakula vya sukari kupindukia, matumizi ya vyakula na mafuta ya mgando yatokanayo na mbegu za mimea kama margarine au vegetable fat. Tafiti zingine zifanyike Tanzania kujua vyanzo vingine vya sumu hizi tusikomee hapa tu watafiti wametugusia vyanzo vya ndani tu.

  1. Watafiti wametuacha njia panda hawajatumbia njia zingine za kujitathimini kiwango cha sumu hizo mwilini na madhara yake yalivyo tokea.

Sayansi inasema kwamba mwili unapokuwa katika msongo wa sumu yaani oxidative stress unakuwa unapata majeraha karibia kila kiungo ndani ya mwili na madhara yake mwili unavimba na unakuwa kwenye mashambulizi. Vita hio inayosababishwa na Free radicals hizo huwa ni vita ya kimya kimya hauvimbi kama vile unapopondwa na jiwe ndio maana kuvimba huku kwa majeraha ndani ya mwili huitwa “Low grade chronic inflammation”.

Unaweza sasa kimaabara ukajichunguza kwa kuchukua sampuli ya damu ukajipima viashiria kwenye damu vinavyo onesha mwili uko kwenye mapambano. Viashiria hivyo ni pamoja na high sensitivity C Reactive Protein, (hs-CRP). Tafiti zinaonesha kwamba hsCRP inaweza kutumika kutoa utathimini wa awali.

 

Mfano. Baba mmoja alifanyiwa upasuaji india wa goti ambalo lilivimba kwa miaka kadhaa na hakuweza kutembea. Alipofika india alipimwa hsCRP ilionekana inasoma 58 na aliporudi Tanzania aliendelea na dawa zake za kutibia goti mpaka akapona vizuri tu. Muda sio mrefu ugonjwa wa presha ikamuanza na hatimaye goti lile la pili nalo likaanza kuvimba kwa kasi sana (Arthritis). Aliponionesha vipimo vyake nikamuuliza je ulibadilisha mfumo wa kula kukabiliana na hili jibu kusoma juu hivi. Mwili wako unatakiwa upozwe utoke kwenye mashambulizi haya mpaka kufikia kiwango kipimo kisome hsCRP 0-5.

 

Mfano wa pili: Mama mmoja alikuja kuniomba ushauri baada ya kupewa namba na daktarin wa mifupa. Alikuwa na presha kali sana na magoti yanavimba sana. Nikamwambia una kisukari? Akasema nimepima sukari ilikuwa 3.8mmol/L hivi. Basi nilipo muona anakosea kutamka majibu ya vipimo nikamwagiza apime hsCRP na apime na Kipimo kikubwa cha sukari HBA1C. Jibu la HBA1C lilikuja 9.2% ina ashiria ni mgonjwa rasmi wa kisukari ila kwa sababu glucometer inasoma 3.8mmol/l nikamwambia wewe ni “Mtahiniwa wa kisukari yaani pre diabetes” nikamwelimisha akanielewa namaanisha nini. Ilipokuja kwenye kiashiria cha mashambulizi ya mwili hsCRP ilikuwa inasoma 19 wakati kawaida inatakiwa isome 0-5. Presha yake ilikuwa kali sana mbali na kutumia dozi kubwa na nyingi za dawa. Na jibu hilo kusoma juu linachangia kupata mashambulizi ya magoti na kupandisha presha.

Hivyo watafiti kidogo wangetupanua namna ya kuweza kujua athari za kuwa kwenye oxidative stress kwenye maabara zetu. Ingawaje jibu ili huwa haliwezi kutumika kuwa kigezo cha mashambulizi kama una mimba, kama una maambukizi yaliyo tokea ndani ya wiki mbili zilizopita. Ila kama yote hayo huna basi kinaweza kukusaidia.

 

  1. Pia kunatakiwa tafiti ifanyike ya kupima Sumu hizo (lipid peroxides) kwenye sampuli za Mafuta kutoka Nyumbani, Hotel na viwandani. Kuna tafiti moja iliyofanyika huko Malaysia na Leong XR alikusanya tafiti mbalimbali ambazo zilikuwa zimefanyika kwa kukusanya sampuli za mafuta mbalimbali ya mbegu za mimea,nazi na mzeituni yaliyotumika majumbani,hotelini na viwandani kukaangia vyakula.( Effects of Repeated Heating of Cooking Oils on Antioxidant Content and Endothelial Function, 2015)

 

Tafiti hii ilionesha kwamba mafuta ya mbegu za mimea yalikuwa yanaongoza katika kiwango cha sumu hizo free radicals kila kila sampuli zilizo chukuliwa sehemu zote. Pia mtafiti ameonesha uhusiano kati ya shinikizo la damu na sumu hizi tunazokula kutoka kwenye vyakula vilivyo kaangiwa mafuta dhaifu kwenye moto. Free radicals huenda kuathiri kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu na kuzuia damu kuweza kutembea katika presha nzuri kwenye mshipa wa damu.

Zoezi la kutanuka na kusinyaa kwa mishipa ya damu husanifiwa au huendeshwa na Nitric Oxide ambayo huzalishwa na mishipa ya damu. Hivyo Free radicals huzuia utengenezaji wa Nitric oxide matokeo yake damu huanza kupita katika presha kubwa sana kule kutanuka kwa mishipa ya damu kunazuiliwa.

Hivyo mtu anapokuwa kwenye msongo wa sumu yaani oxidative stress anakuwa hatarini sana  kupatwa na shinikizo la damu. Mbali na hivyo tafiti imeonesha kwamba Free radicals husababisha majeraha kwenye kuta za mishipa ya damu (Endothelial injury) ambazo huhatarisha mrundikano wa lehemu kwenye kuta za mshipa wa damu.

Nilipo Ona Tafiti ya Kimaabara tena imefanyika muhimbili inahusisha “Oxidative stress” na Magonjwa ya moyo kwa Mtu mwenye Kisukari nilifarijika sana.

 

Wana falsafa wanasema

Wanasema Kuutibu ugonjwa huwa hakuhitaji umakini mkubwa kama kuuzuia ugonjwa. Yaani Ukitaka Kujikita Kuwakinga watu na maradhi mbinu zako zinatakiwa ziwe imara kuliko nyenzo unazotumia kuutibu ugonjwa”.

 

  1. Kama Tafiti imeonesha kimaabara kwamba Wagonjwa wenye Kisukari, Presha kali na magonjwa ya moyo wameonesha kuwa na Free Radicals nyingi kuliko wale wazima. Je kifanyike nini kuwakinga watu na Janga hili?

 

Mfano: Wagonjwa wengi waliohudhuria kliniki siku hio sukari ilikuwa zaidi ya 10mmol/L na hapo hawakupimwa kipimo kikubwa HbA1C. Ina maana Ukitaka kuwakinga watu wasipate maradhi yanayo pandiliana (Ugonjwa mmoja mzito juu ya mwingine)ni “Kuongeza Nyenzo Katika kudhibiti Sukari isipande”. Ingawaje tafiti haijatoa ushauri wowote nini kifanyike katika kliniki ya wagonjwa wenye kisukari ili kuhakikisha kwamba sukari inadhibitiwa na tupunguze majanga ya kisukari. Bado kuna changamoto na mjadala mkubwa sana katika mbinu mbadala za kuzuia majanga ya kisukari kama nilivyo eleza katika kitabu cha Nuru ya Kisukari. Juhudi binafsi ya mgonjwa kwa sasa ndio inahitajika kusoma na kuelewa ugonjwa na kuchukua hatua.Related image

  1. Tizama Picha Hii kushoto jinsi mwili unavyo Angamizwa pale unapokuwa kwenye msongo wa sumu. Tafiti hii naona kama imetufungua macho kutuonesha uhusiano wa maradhi sugu ya lishe na sumu hizi. Sasa Inatakiwa Tuumize kichwa tuvijue vyanzo vingine vya Oxygen Free Radicals. Maradhi Mengi tunayo sugua Benchi mahospitalini yawezakuwa una Msongo wa sumu hizi.

 

  1. Kuna Tafiti nyingi zinazo Onesha kwamba Mafuta ya mbegu za Mimea (Alizeti,Soya,Pamba,Mahindi) ni Dhaifu kwenye moto wakati wa kukaangia chakula. Na Huzalisha Hizi sumu nyingi kuliko mafuta mengine kama Samli,Siagi,Nazi nk. Ukila samaki,Nyama,Broila,Chips Viazi Mihogo iliyokaangwa kwenye mafuta dhaifu kwenye moto kama mbegu za mimea zile Free Radicals hupenya na kuwa sehemu ya chakula wakati wa kukaanga.

 

Chakula cha mfumo huo Kinamhatarisha mtu kuwa kwenye msongo wa sumu “Oxidative stress”. Sasa Kama tumeona tafiti inatuonesha uhusiano wa “Oxidative stress na Mrundikano wa lehemu kwenye mishipa ya moyo” Ina maana Kumwambia mtu mafuta mazuri “Ni mbegu za mimea Unamhatarisha. Huku ana kisukari siku zote akila ngumi inasoma juu, Huku anakula mihogo imekaangwa na mafuta ya alizeti ya tangu juzi. Anakula nyama nyeupe ya mafuta ya juzi..! Halafu tunasema “Kisukari ni ugonjwa sugu usiotibika” …Ukikupata unakufa nao..! Adui hatujawajua dhahiri..!

 

 

Hizi ni mbinu 10 za kudhibiti Ugonjwa wa kisukari

  1. Usiweke mwilini Chakula Kingi ambacho mwili Umegomea. SUKARI na WANGA

  2. Furahia vyakula vyenye mafuta ASILI na Kiwango Kingi cha Omega 3 na mafuta yanayo himili moto. Tumia Siagi,Nazi,Samli,olive oil nk i

  3. Kula vyakula unavyo ruhusiwa katika SAYANSI YA MAPISHI kwa Uhuru mpaka USHIBE. Kama Mboga za majani,samaki,matunda yenye sukari kidogo,mayai nk

  4. Kula tu pale unapojisikia Njaa na Unaposhiba SITISHAkula

  5. PimaSUKARI YAKO Kabla hujanywa dawa ya sukari

  6. Usiache dawa zako Gafla kabla afya yako haijaimarika au Daktari hajajiridhisha na Vipimo vya sukari

  7. Weka Kumbukumbu ya sukari yako Kila siku. Wiki ya kwanza Pima mara tatu kwa siku. Huu ni USHAHIDI TOSHA

  8. PimaHemoglobin A1C kila  baada ya miezi mitatu mpaka itakaposoma 5.7% utakuwa sio Mgonjwa wa Kisukari tena

  9. Fanya mazoezi angalau mara mbili kwa wiki. Hakikisha kwa siku nzima kila siku unatembea Dakika 150. MASAA MAWILI NA NUSU.

  10. Pombe,Mvinyo aina yoyote, na Juisi aina yoyote Huruhusiwi Kutumia unachelewesha majibu 

     

    HABARI KWA HISANI YA DR BOAZ MKUMBO 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!