MAMA KAUZU; Ohhhh! Hakuna shida, inamaana bado hujajifungua, maana niliona picha za mtoto nikajua tayari ushajifungua, au wewe Sio Salma wa mwanza yule nilofumania video zenu za uchi.
HALIMA; Hapana mimi sio salma mimi ni Halima, huyo Salma mimi simjui najua nitaolewa mimi mke mwenzako ulijue hili.
MAMA KAUZU; Ohhh! Kumbe Halima, wewe si ndiyo yule wa Tabora mume wangu alitoroka kazini kuja kwenu kujitambulisha?
HALIMA; Hapana mimi wa Shinyanga mume wetu bado hjajajitambulisha ameniambia nikijifungua ndiyo anajitambulisha.
MAMA KAUZU; Ohhh, kumbe Halima wa Shinyanga, basi nikuambie shogaa, kwenye michepuko yetu yote wewe ndiyo nilikupenda maana mzuri mweupe, afadhali umebeba mimba nyingine maana niliposikia umetoa ila mimba ya kwanza roho iliniuma sana…
HALIMA; Mbona wewe Mama unanichanganya, mimi sijawahi kutoa mimba ya mume wako, mume wako nina mahusiano naye huu mwezi wa nne na kaniambia atanioa, wewe unamsumbua sasa hao wengine unaonitajia ni kina nani mbona aliniambia niko peke yangu.
MAMA KAUZU; Hao wengine ni michepuko yetu Dada yangu, uwe peke yako umekua moyo wewe, Figo zenyewe ziko mbili, Bibie kama alikudanganya uko peke yako ukamzalia basi jua imekula kwako, tuko wengi na wote tuna vizazi tumemzalia, wewe zaa ukishindwa kulea tuletee tutakulelea….
HALIMA; (Akakata simu)
No comments:
Post a Comment