Friday, 21 August 2020

NECTA yatangaza matokeo ya Kidato cha Sita kwa mwaka 2020. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 0.03

 1.jpg

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania, limesema watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa 84,212 waliofanya mtihani kidato cha sita Juni/Julai 2020 wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde amesema, watahiniwa 85,499 walisajiliwa kufanya mtihani huo.

Amesema, kati yao wasichana walikuwa 36,168 sawa na asilimia 42.30 na wavulana walikuwa 49,331 sawa na asilimia 57.70.

Dk. Msonde amesema, kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 74,753 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 10,746.

Amesema, kati ya watahiniwa 85,499 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 84,212 sawa na asilimia 98.49 walifanya mtihani na 1,287 sawa na asilimia 1.51 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ugonjwa na utoro.

Katibu mtendaji huyo amesema, watahiniwa wa shule, kati ya 74,753 waliosajiliwa, watahiniwa 74,284 sawa na asilimia 99.37 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 32,403 sawa na asilimia 99.60 na wavulana 41,881 sawa na asilimia 99.19.



Kuangalia maokeo, fungua https://matokeo.necta.go.tz/acsee/index.htm

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!