Monday, 24 August 2020

Maumivu ya mgongo na jinsi ya kuyazuia

 

Maumivu ya mgongo ni moja kati ya matatizo makubwa sana yanayoathiri watu wengi katika miaka ya hivi karibuni. Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimethibitisha kuwa, maumivu ya mgongo hujitokeza zaidi miongoni mwa watu wa umri wa kuanzia miaka 25-40 na kuendelea. 


Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja ya chanzo cha maumivu ya aina hii, inaaminiwa kuwa huenda maumivu haya yanatokana na majeraha katika misuli au mifupa ya uti wa mgongo.

 Katika idadi ya waathirika wa maumivu hayo, wapo wanaopata maumivu makali sana ya muda mrefu kiasi kwamba, wanashindwa kufanya shughuli za kawaida, vilevile wapo ambao hupata maumivu ya mgongo ya muda mfupi tu. Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja ya chanzo cha maumivu ya aina hii, inaaminiwa kuwa huenda maumivu haya yanatokana na majeraha katika misuli au mifupa ya uti wa mgongo. 

 Maumivu ya mgongo yanaweza kusababishwa na ujauzito; na maumivu haya huongezeka zaidi kadri mtoto anavyokua.

Vitu vinavyosababisha  maumivu ya mgongo mara nyingi huletwa na tabia ya kuinua vitu vizito kwa muda mrefu, mfano kuinua vyuma, kubeba ndoo au mitungi ya maji kichwani hasa kwa wanawake. Kukaa au kusimama kwa muda mrefu pia kunaweza kuwa chanzo cha maumivu haya. 

Kwa wanawake, maumivu ya mgongo yanaweza kusababishwa na ujauzito; na maumivu haya huongezeka zaidi kadri mtoto anavyokua. Zaidi ya hayo, maumivu haya pia yanaweza kusababishwa na kuwa na maambukizi katika uti wa mgongo, mfano maambukizi ya Kifua Kikuu (TB) ya uti wa mgongo. 

Vyanzo vingine vya maumivu haya ni kuwa na uzito mkubwa wa mwili, kuwa na ngiri katika pingili za uti wa mgongo na kupata majeraha au ajali maeneo ya mgongo. 

 Dalili na jinsi ya kujikinga nayo Jinsi ya kuepuka maumivu haya ya mgongo yanaweza kuepukika kirahisi ikiwa hatua zinazofaa zitachukuliwa. Mfano; Kuacha matumizi ya sigara, Kuepuka kulala kifudifudi na chali Kupunguza uzito wa mwili, Kuepuka kubeba uzito mkubwa, Kuepuka kuvaa nguo zenye kubana sana, Kuepuka kuvaa viatu vyenye visigino virefu, Kuepuka kuinama wakati wa kunyanyua vitu vizito (kuchuchumaa ni bora), na Kubadili mfumo wa maisha kama vile kuepuka kukaa kitako au kusimama kwa muda mrefu. 

Pia wagonjwa wanaweza kukandwa mgongo kwa kutumia mafuta maalumu ili kulegeza misuli ya pingili za uti wa mgongo, kulalia magodoro maalumu kwa wanaoumwa na mgongo, na kuhakikisha kufanya mazoezi ya kunyoosha mgongo.



 Makala yameandikwa na Daktari Ali Hassan, daktari binafsi, Nairobi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!