Monday, 6 July 2020

Madascar yaweka amri ya kutotoka nje kufuatia ongezeko la Corona

35 Interesting Facts About Madagascar | Madagascar flag ...
Rais wa Madagasca alitangaza dawa ya kunywa ya mitishamba inayotokana na mmea wa pakanga pamoja na mimea mingine inayoweza kutibu maambukizi ya virusi vya corona.


Madagascar imeuwekea mji wake mkuu Antananarivo amri ya kutotoka nje kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya virusi vya corona, miezi miwili baada ya masharti hayo kuondolewa, ametangaza rais.
Katika taarifa, eneo la Analamanga ambalo ndilo lenye mji mkuu linafungwa tena, rais alisema.
''Hakuna magari yatakayoruhusiwa kuingia ama kutoka katika eneo hilo kuanzia leo Jumatatu hadi Julai 20 na masharti makali yatawekewa wanaotoka''.
''Ni mtu mmoja mmoja katika kila familia atakayeruhusiwa kwenda barabarani kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa sita mchana'', ilisema taarifa hiyo.
Hatua hizo zimechukuliwa kutokana na kusambaa kwa mlipuko huo na kuongezeka kwa visa vya Covid-19, iliongezea.
Madagascar ilikuwa imezoea kuandikisha visa vichache kwa siku vya ugonjwa huo lakini sasa ,taifa hilo katika siku za hivi karibuni limwthibitisha idadi kubwa ya wagonjwa wa Covid 19 kila siku , ambapo wagonjwa 216 waliripotiwa siku ya Jumamosi baada ya watu 675 kupimwa.
Takriban watu 24,000 wamepimwa virusi hivyo kuafikia sasa.
Tangu virusi hivyo vilipogunduliwa katika kisiwa hicho Machi 20 , taifa hilo lilikuwa na jumla ya wagonjwa 2,728 ikiwemo watu 29 waliofariki kufikia siku ya Jumapili.
(Bbc Swahili)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!