Shirika la afya Duniani WHO limesema kuwa maambukizi ya Virusi vya Corona yanaongezeka duniani, mpaka hapo jana watu wengine zaidi ya laki mbili waliongezeka miongoni mwa walioambukizwa katika muda wa saa 24.
Shirika la WHO limesema mpaka sasa watu zaidi ya Milioni 10 wameambukizwa Virusi hivyo duniani kote na zaidi ya laki tano wameshakufa.
Marakeni ndiyo iliyokumbwa na zaidi ya nusu ya maambukizi yote yaliyotokea katika saa 24 zilizopita, ikifuatiwa na Brazil., asasi hiyo ya afya pia imeripoti kwamba nchi za kusini mashariki mwa Asia zinashika nafasi ya pili kwa idadi ya maambukizi duniani.
MillardAyo.com
MillardAyo.com
No comments:
Post a Comment