Watu wengi huenda hawajui kama kukoroma ni ugonjwa. Kukoroma ni ugonjwa unaosababisha mtoto au mtu mzima kuacha kupumua akiwa usingizini hivyo anakuwa anashtuka na hivyo kushindwa kupata usingizi mzuri.
Wataalam wenyewe wanaita (Obstructive Sleep Apnea (OSA)). Hali hii ina madhara makubwa kwa mtoto. Haya ni baadhi ya madhara hayo
inaweza kusababisha mtoto kuwa mtukutu, mchokozi kukosa utulivu na kukurupuka anapofanya mambo yake
kulala lala wakati wa mchana
kushindwa kukuwa na kuongezeka uzito sawasawa -wengi baada ya matibabu huwa wanakuwa na kuongezeka uzito
madhara kwenye mapafu na moyo ikiwemo moyo kufeli.
Sasa iwapo mwanao anakoroma mara kwa mara (angalau siku 3 kwa wiki) ama anakoroma kwa sauti na wakati mwingine unamuona kabisa anaacha kupumua, muone daktari wa pua na koo kama upo sehemu ambako wanapatikana. Sababu mojawapo kwa watoto wengi ni kuvimba kwa nyama za pua (adenoid) na mafindofindo(tonsil). Ukimuona daktari atakushauri tiba ipi inafaa.
Picha inaonyesha mtoto mwenye mafindofindo(tonsil)makubwa ambayo yanaweza kuziba kwa urahisi njia ya hewa na kusababisha mtoto kukoroma.
No comments:
Post a Comment