"Siwezi kuwateua Watu kisha Wamekaa wanabishana tu ndiyo maana nimesema RC,DC, DED Arusha wapumzike kwanza na hili liwe fundisho kwa viongozi niliowateua, mkajenge element za kuvumiliana kama unataka kubishana nenda kabishane nyumbani kwako na Mke wako" - JPM
“Mkuu wa Mkoa Arusha ukasimamie migogoro, kuna migogoro mingine inatengenezwa makusudi, kaisimamie vizuri, mfano kulikuwa na mgogoro pale wa kanisa na shule kuna maamuzi hayakuwa ya kweli, nikawaambia wakitaka eneo wajenge ghorofa,Jiji haliwezi kuingia gharama kutafuta eneo”-JPM
•
•
“Kulikuwa na mgogoro wa Msikiti Arusha, eneo lao ni mita za mraba 10,495 na open space mita 4165, kuna kiongozi mmoja akawa anawaambia ombeni na hili eneo DED alipokataa shida, ni kumchonganisha DED na Waislamu na hili lilianza tangu enzi za Mwinyi,Mkapa, Kikwete wakakataa na mimi msimamo wangu ni uleule nakataa”-JPM
•
“Tatizo hili (la migogoro Arusha) lililetwa na Mkuu wa Mkoa Arusha(Gambo) anazungumza hivi huku, anazungumza hivi kule lengo ni kuonekana yeye ni mzuri sana, tusitoe ahadi ambazo haziwezekani lazima tusimamie Sheria, RC, DC msiende kuingia kwenye matatizo”-JPM#MillardAyoUPDATES

No comments:
Post a Comment