Thursday 28 May 2020

Trump aguswa na kifo cha George Floyd

US: Trump says federal social distancing guidelines won't be ...
Rais Donald Trump amesema tayari ameagiza uchunguzi kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd ambaye amefia mikononi mwa Polisi, Trump amesema atapokea ripoti ya uchunguzi leo na hatua zaidi zitachukuliwa”natoa pole tena kwa Familia, Watu wawe watulivu kila kitu kitakuwa sawa”

Waandamanaji mjini Minneapolis Marekani wameendelea kupambana na Askari kwa siku ya pili mfululizo wakishinikiza Polisi waliosababisha kifo cha George Floyd wafikishwe Mahakamani, Rais Trump a
mesisitiza kuwa ripoti ya uchunguzi itatoa mwanga na haki itatendeka.

Watu mbalimbali wameshikwa na hasira baada ya video kusambaa zikimuonesha Polisi mweupe akimkanyaga shingoni kwa goti Floyd huku akilalamika kukosa pumzi hadi kupelekea kifo chake, Polisi huyo na wenzake watatu wamefukuzwa kazi lakini Watu wanasema kufukuzwa kazi pekee haitoshi.

#MillardAyoUPDATES

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!