Thursday 21 May 2020

Mobeyto-Maisha ni majira!.

Verified




Ukifika wakati wa KUACHANA sio lazima MGOMBANE.
Kuna wakati itabidi uachane na mbia wako (Business Partner) wa biashara ambaye mlipanga kufika mbali sana.



Kuna wakati itabidi uachane na bosi wako ambaye ndiye alikusaidia kukufundisha kazi hapo mwanzo.
Kuna wakati itabidi uachane na mtu uliyekuwa unampenda sana na ulidhani utakuwa naye kwa muda mreeefu.

Kuna wakati katika maisha utalazimika kuachana na watu, ofisi.... n.k.
Ukifika wakati huu kuna mambo ya kuzingatia.
Moja, sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao.
Unaweza kuachana kwa HESHIMA na UTULIVU.
Kumbuka kuachana sio VITA, mnaweza kuachana na maisha yakaendelea.
Sio lazima uwageuze ADUI wale unaowaacha au wanaokuacha.
Maisha yana majira na kila mtu anatakiwa kuwa mahali fulani kwenye majira tofauti.
Mbili, pokea maumivu na yakubali. Haitasaidia kutokubali uhalisia.

Kama mtu ameamua kuondoka, hakuna namna.
Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa hatua inayofuata.
Tatu, usijilazimishe kuonyesha ubaya wa unayeachana naye.

Kumbuka mafanikio ya UNAKOKWENDA hayajabebwa na watu kujua ubaya wa UNAYEACHANA naye bali yamebebwa katika DHAMIRA SAFI ya UNACHOKWENDA KUFANYA.

Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unayeachana naye.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!