Anaitwa FĂ©licien Kabuga alikuwa ni mfanyabiashara maarufu nchini Rwanda kabla ya kufanyika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Alizaliwa katika eneo la kaskazini mwa Rwanda ambako alijilimbikizia mali kutokana na biasahara ya majani ya chai miaka ya 1970 na kuwekeza katika biashara tofauti nchini humo, mataifa jirani na ng'ambo. Alikuwa mwandani wa karibu wa chama tawala cha MRND na baba mkwe wa Rais Juvénal Habyarimana.
Kabuga anayetuhumiwa kuwa mfadhili mkuu wa mipango ya kutekeleza mauaji ya kimbari, alikuwa mmliki wa kituo cha radio ya kibinafsi RTLM ambacho kililaumiwa kwa kuwahamasisha watu wa jamii ya Kihutu kuwaua wenzao wa Watutsi.
Kutokana na utajiri wake na connection ulimwenguni, baada ya mauaji ya kimbari Kabuga alitoroka Rwanda na kukimbilia Ulaya, alijificha Asnières-Sur-Seine nchini Ufaransa, akatimia ujasusi kubadili majina yake na mambo kadhaa ya kibaolojia katika sura yake. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, Ufaransa, Ubelgiji na kwingineko, waliweka madau makubwa kwa yeyote atakayefanikiwa kukamatwa kwake, lakini ilishindikana kwa miaka 26.
Mwamba huyu ameichezesha dunia vilivyo, ameweza kujificha kwa miaka 26 tangu mauaji hayo, ambapo 15/5/2020 usiku, Shirika la Ujasusi la Ufaransa lilifanikiwa kumkamata akiwa tayari ni mzee kikongwe wa miaka 84 sasa, yaani akiwa ni wakuanika na kumwanua juani, anatembelea kiti tu mjini Asnières-Sur-Seine nchini Ufaransa.
Hebu fikiria shiirika la Ujasusi Ufaransa la DGSE linalosifika kwa ujasusi ulimwenguni ambalo lilifanikiwwa kumkamata Carlos Ramirez Sanchez 1994 nchini Sudani. Lakini limecheza kwa miaka 26 kufanikiwa kugundua mtu kama FĂ©licien Kabuga ambae alikuwa kajificha ndani ya Ufaransa hiyo hiyo.
Anaweza kuletwa mjini Arusha, Tanzania katika mahakama ya kimaita inayosikiliza kesi za mauaji ya Kimbari.
CHANZO: JMF.
No comments:
Post a Comment