Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha linamshikilia Daniel Emmanuel (32) Mkazi wa Sakila wilayani Arumeru, kwa kukutwa akinywa damu ya mama yake Mzazi Eliyamulika Emmanuel Sarakikiya (79) kwenye kikombe, baada ya kumuua kwa shoka na kutenganisha shingo,mkono na mguu na kiwiliwili.
"Mtuhumiwa alimkata kwa shoka shingoni mama yake na kutenganisha na mwili wale na akaona haitoshi akakata mguu wa kulia na kuutenganisha na akakata mguu wa kushoto pia akautenganisha wakati anafanya unyama huu alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa,"amesema Kamanda Shana.
No comments:
Post a Comment