Sunday 26 April 2020

Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona


Corona...
Taarifa Muhimu:
Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona

0800110124
0800110125
Namba hizi kupiga Ni bure hata kama hauna salio kwenye simu yako.


DALILI ZA UGONJWA WA CORONA
Dalili zionekanazo mara kwa Mara:
• Homa
• Kikohozi kibichi
• Uhemaji wa tabu
• Maumivu ya mwili
• Kuuma kwa koo mfano wa
matonses (tonsillitis)
• Kukosa hamu ya kula
Dalili za mara chache:
• Kuhara
• Kutapika
• Kichwa kuuma
• Kukohoa damu
• Maumivu ya kifua
Nani hupatwa na korona?
• Watu wote (wakike kwa kiume) waweza
kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.
KINGA:
• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa
Kirusi cha korona katika mwili wa
binadamu:
• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!