Wizara ya Afya Tanzania kupitia Waziri Ummy Mwalimu imetoa taarifa juu ya uwepo wa wagonjwa watano wa corona ambao wote ni Watanzania na wakazi wa DSM, pia Waziri wa Afya Zanzibar ametangaza wagonjwa wapya wawili, hivyo waliothibitika kuwa na corona Tanzania hadi sasa ni 32 ambapo kati ya hao watano wamepona na 24 wanaendelea vizuri na matibabu, Ummy amesema pia vimeongezeka vifo viwili na kufanya idadi ya vifo kufikia vitatu.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo leo April 10,2020 kuna jumla ya maambukizi 32 Tanzania, vifo vitatu, maambukizi mapya 7, wagonjwa waliopona na kuruhusiwa 5, Watu 280 wanafuatiliwa kwa kuwa karibu na wagonjwa corona, waliomaliza ufuatiliwaji 461 na wasafiri waliopo karantini 210.
CHANZO: MillardAyo.com
No comments:
Post a Comment