Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa 14 wa corona wameongezeka na kufanya idadi ya visa vya corona Tanzania kufikia 46 kutoka 32, wagonjwa wapya wote ni Watanzania, kati yao walioko DSM ni 13 na mmoja yuko Arusha, wagonjwa wote wanaendelea na matibabu.
Kwa mujibu wa takwimu za jumla za corona kutoka Wizara ya Afya Tanzania leo April 13,2020 kuna jumla ya maambukizi 46, vifo vitatu, maambukizi mapya 14, wagonjwa waliopona na kuruhusiwa 7, Watu 590 wanafuatiliwa kutokana na kuwa karibu na wagonjwa corona, waliomaliza ufuatiliwaji 413 na wasafiri waliopo karantini 84.
CHANZO: MillardAyo
No comments:
Post a Comment