Monday, 30 March 2020
Wagonjwa wa CoronaTanzania waongezeka na kufikia 19
Waziri Ummy Mwalimu akitoa taarifa juu ya mwenendo wa Virusi vya Corona nchini amesema leo asubuhi wamepokea vipimo vya wagonjwa watano kutoka maabara ya taifa, watatu wanatoka Tanzania Bara na wawili wakitokea Zanzibar.
Idadi imefikia 19 akiwepo mgonjwa mmoja aliyetangazwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar Machi 28, 2020.
Ninakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment