Sunday 15 March 2020

Serikali ya Tanzania yasema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Corona"


Serikali imesema hadi sasa hakuna taarifa za mgonjwa wa Corona aliyebainika hapa nchini na imewataka wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambazwa na watu katika mitandao ya jamii kuwa kuna watu wamebainika na kupelekwa katika maeneo maalum.



Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo, Dakta Hassan Abbas akizungumza Jijini Dodoma amesema, Tanzania bado iko salama.
Dakta Abbas amesisitiza kuendelea kuchukua hadhari ya kujikinga na kufafanua kwamba katika maeneo yanayotumiwa na wageni kuingia hapa nchini, yamewekwa vifaa maalum kwa kupima joto la mwili na sio Corona.

ITV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!