Sunday 8 March 2020

Maneno kuntu kwa siku ya Wanawake toka kwa Magid Mjengwa


Kwenye Siku Hii Ya Wanawake Tumtafakari House Girl/ Child Huyu...
Ndugu zangu,
Imepata wiki sasa nimeweka mezani moja ya changamoto za kijamii ambazo kwa bahati mbaya tumechagua kutoizungumzia hadharani.


Inahusu wafanyakazi wa majumbani. Yawezekana msomaji unaye mmoja nyumbani kwako. Yawezekana unampa haki zake kama sheria ya kazi inavyotaka.
Hata hivyo, ukweli ni kuwa wengi wa wafanyakazi hawa wa ndani wanaishi kwenye hali ya ubaguzi na unyanyasaji mkubwa.
Ona, House girl/ Child ni wa kwanza kuamka, wa mwisho kulala. Analala wapi? Hana Jumamosi wala Jumapili ya kupumzika. Hana likizo. Hana Bima ya Afya wala NSSF pindi akiacha kazi au kufukuzwa ili imsaidie. Hana mkataba wa kazi.
Nini kifanyike?
Ni wakati sasa ikapitishwa sheria ya Bunge ya kuwepo kwa chombo cha kuratibu ajira hizi za majumbani kwa minajili ya kulinda haki za wafanyakazi hawa na kudhibiti ajira za watoto ( Child labour).
Ni wakati pia, kwa vituo vya polisi kutumia dawati la jinsia kama dawati pia la kusikiliza kero na mashauri yenye kuhusu unyanyasaji wa wafanyakazi wa majumbani.
Inawezekana.
Happy Women’s Day!
Maggid

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!