Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.
Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
=====
MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO
Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi
Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
No comments:
Post a Comment