Wednesday 29 January 2020

Maambukizi ya Virusi vya Corona vifo 81 wagojwa 4535


Idadi ya waliofariki kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini China imeongezeka na kufikia Watu 81 huku idadi ya Wagonjwa kwa China pekee ikifikia Watu 4535 .

Biashara kubwa China zimefungwa au Waajiriwa kupewa muongozo wa kufanyia kazi majumbani ili kupunguza ugonjwa kuenea zaidi, Watu hawajaacha kuvaa mask kila wanapokwenda ili kujikinga na maambukizi.

Unaambiwa Wataalamu wanasema idadi ya waliothirika inaweza kuwa kubwa zaidi, Nchi nyingine zenye Wagonjwa wa Virusi hivyo ni Thailand 8, Australia 5, Marekani 5, Singapore 5, Malaysia 4, Japan 4, Korea Kusini 4, Ufaransa 3, Canada 2, Vietnam 2 ,Ujerumani 1, Nepal 1, Sri Lanka 1 na Cambodia 1.
#MillardAyoUPDATES

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!