Thursday 9 January 2020

𝐇𝐚𝐫𝐫𝐲 𝐧𝐚 𝐦𝐤𝐞𝐰𝐞 𝐌𝐞𝐠𝐡𝐚𝐧 𝐤𝐮𝐭𝐚𝐧𝐠𝐚𝐳𝐚 '𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚' 𝐤𝐮𝐣𝐢𝐡𝐮𝐬𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐡𝐮𝐠𝐡𝐮𝐥𝐢 𝐳𝐚 𝐤𝐢𝐟𝐚𝐥𝐦𝐞.

𝐅𝐚𝐦𝐢𝐥𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐟𝐚𝐥𝐦𝐞 𝐲𝐚 𝐔𝐢𝐧𝐠𝐞𝐫𝐞𝐳𝐚 𝐢𝐦𝐞𝐬𝐢𝐤𝐢𝐭𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐦𝐟𝐚𝐥𝐦𝐞 𝐇𝐚𝐫𝐫𝐲 𝐧𝐚 𝐦𝐤𝐞𝐰𝐞 𝐌𝐞𝐠𝐡𝐚𝐧 𝐤𝐮𝐭𝐚𝐧𝐠𝐚𝐳𝐚 '𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚' 𝐤𝐮𝐣𝐢𝐡𝐮𝐬𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐡𝐮𝐠𝐡𝐮𝐥𝐢 𝐳𝐚 𝐤𝐢𝐟𝐚𝐥𝐦𝐞. 𝐊𝐚𝐬𝐫𝐢 𝐥𝐚 𝐁𝐮𝐜𝐤𝐢𝐧𝐠𝐡𝐚𝐦 𝐢𝐦𝐞𝐡𝐮𝐳𝐮𝐧𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳𝐢 𝐡𝐚𝐲𝐨 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐡𝐚𝐢𝐤𝐮𝐡𝐮𝐬𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐥𝐚 𝐡𝐚𝐢𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐫𝐢𝐟𝐚 𝐳𝐨𝐳𝐨𝐭𝐞 𝐳𝐚 𝐚𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐤𝐮𝐡𝐮𝐬𝐮 𝐦𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐝𝐨𝐚 𝐡𝐚𝐨.

BBC imebainisha kuwa si Malkia wala mwana mfalme William au waandamizi wengine katika falme walijulishwa hatua hiyo na kwa kwamba uongozi wa juu wa ufalme umepata pigo. Kasri ya kifalme imesema kuwa suala hili ni gumu sana na wamelipokea kwa mshtuko mkubwa.

Katika maelezo yao, Harry na Meghan walisema kuwa walifikiria uamuzi huo kwa muda mrefu na kufanya maamuzi hayo miezi mingi iliyopita. Harry na Meghan wamepanga kugawa muda wao kwa nusu kuishi Marekani na nusu Uingereza kuendelea kumtumikia malkia na kujihusisha na shughuli za kifalme > "Maamuzi hayo yataturahisishia kumlea mtoto wetu katika makuzi ya utamaduni wa kifalme, na kuipa fursa familia kuangalia hatua inayofuata,".

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!