Sunday 24 November 2019

DR Congo: Takriban watu 28 wamefariki baada ya ndege kuanguka katika makazi ya watu

Image may contain: one or more people and outdoor
 Wamefariki Mashariki mwa Nchini hiyo baada ya ndege iliyokuwa na Watu 18 (Abiria 16 na Rubani 2) kuanguka katika Makazi ya Watu na kuua waliokuwemo ndani ya ndege na Wakazi 10



Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Goma, kwenye mtaa wa Birere wenye watu wengi karibu na mpaka wa Congo na Rwanda,
Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu wangapi walikufa na wangapi walijeruhiwa

Zoezi hilo linafanyika kwa msaada wa wananchi wa mji huo ambao waendelea kupekua nyumba za majirani zilizo angukiwa na ndege hiyo ya kampuni ya Beesyby

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya safari zake huko Kivu kaskazini ikisafiri kati ya miji ya Goma, Butembo na Beni.

Waziri wa Afia Kivu Kakule Kanyere Moise anasema kwa sasa ni mapema kusema watu wangapi waliofariki lakini mwandishi wetu Austere Malivika alishuhudia miili kumi na sita katika sehemu ya tukio na manusura mmoja.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!