Saturday, 17 August 2019
Fahamu kuhusu ugonjwa wa Kiharusi Dalili na Tiba
Kiharusi ni mabadiliko yanayo tokea kwa kasi katika eneo la ubongo /ubongo wote ambayo dalili zake huduma kwa muda zaidi ya masaa 24 na chanzo chake ni ubongo kukosa hewa ya oxygen kutokana na mishipa ya damu eneo la ubongo kupasuka(cerebral haemorrhage) ama kusinyaa (cerebral infarction)[WHO]
Dalili za awali
1.Maumivu ya kichwa kama umepigwa na nyundo (siku nzima/masaa mengu ya siku)
2.Kupata shida ya kuona/kuona vitu viwili viwili au kuona giza
3.Mdomo kuenda upande
4.Kukosa nguvu ya mkono au mguu upande mmoja au kushindwa kuinuka au kudondoka chini wakati unatembea
5. Kupoteza fahamu au kufariki
Kiwago cha athari kutoka repoti ya WHO
Takribani watu milioni 15 wanapata tatizo la kiharusi kila mwaka miongoni mwao milioni 5 hufariki milioni 5 hubaki na ulemavu wa kudumu
Pia kiharusi ni chanzo cha 2 cha vifo dunia nzima na chanzo cha 3 cha ulemavu dunia nzima asilimia 70% ya kiharusi vinavyotokea duniani hutokea kwenye nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati.
Kwa takribani miongo 4 (miaka 40) iliyopita nchi zilizo endelea zimefanikiwa kupunguza idadi ya watu wapya wanao pata kiharusi kwa asilimia 42%. Wakati idadi ya wahanga wapya imeongezeka mara 2 katika nchi zenye uchumi wa chini na wakati.
Kwa Tanzania idadi kamili za wahanga nimeshindwa kuzipata kutokana na ukosefu wa takwimu zilizofanyiwa uchunguzi na kuchapishwa ila kutokana experience yangu idadi ya wahanga wa ugonjwa huu imeongezeka kwa kasi sana na kuwapata hadi vijana wenye umri mdogo.
MADHARA YANAYOTOKANA NA KIHARUSI
1. Kupooza kwa upande mmoja wa mwili
2. Kupoteza uwezo wa kumeza au kutafuna chakula na kupelekea mtu kulishwa kupitia nasogastric tube(NGT)
3. Kushindwa kuongea au kuongea kwa shida
4. Kupoteza kumbukumbu (kusahau) na kushindwa kuconcetrate
5.Ukakamavu wa misuli na viungo
6. Ulemavu wa muda mfupi au wakudumu
7.Msongo wa mawazo kwa mhanga na wanafamilia.
8. Kifo
ATHARI KITAIFA
1. Kupotea na kupungua nguvu kazi ya uzalishaji
idadi kubwa ya wahanga ni watu wenye mchango mkubwa katika uzalishaji wa taifa kwahyo taifa linapata hasara ya kupoteza rasilimali watu katika njanja mbali mbali za uzalishaji.
2. Ongezeko la umasikini kwa familia na taifa kiujumla
wahanga wengi ni nguzo ya utafutaji kifamilia.(Baba /mama/mume/mke)
akipata kiharusi familia inazoroteka kiuchumi . Pia inachangiwa na gharama kubwa za kumhudumia mhanga wa kiharusi. Na wenza kuacha kazi au shughuli za kiuchumi na kumhudumia mgonjwa
3. Matatizo ya kiafya kwa wanafamilia
mfano maumivu ya mgongo katika shughuli za kumbeba na kumgeuza mgonjwa
4.Mifarakano katika Ndoa na Familia
wenza kuwakimbia wenza wao pale wanapopata tatizo hili au kuwanyanyapaa
wanandugu kukimbia majukumu ya kumsaidia mgonjwa na familia yake
NINI KIFANYIKE? kupunguza na kukabili hili tatizo la kiharusi
1. TUBADILI MITINDO YA KIMAISHA
¡. Kupunguza au kuacha matumizi ya vilevi/sigara kupita kiasi au kila siku
¡¡. Kujifunza na kujizoesha tabia ya mazoezi mara 5 kwa wiki . kila siku kwa muda usiopungua dakika 30.
¡¡¡. Kuzingatia milo sahihi
- Hasa kiwango cha chakula kisizidi sana mfano mtu anakula ugali kilo 1 peke yake.
mwili unahitaji kiwango fulani kidogo cha nguvu kutoka kwenye huo ugali mfano labda robo ya ugali. hiyo nusu na robo inayobaki huhifadhiwa kwenye mwili kama mafuta na kukuweka katika hatari ya kupata tatizo la presha na kiharusi
-Kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga mfano chapati,maandazi,keki,ugali,wali,mikate nakadhalika
-Kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta mfano mlo sahihi si kula vitu vuzuri au vitamu tamu. Bali ni kuzingatia makindi saba ya chakula. hakikisha chakula chako cha kila siku kina atleast makundi 4 ya chakula/virutubisho
2.KUONGEZA VIWANGO VYA SHUGHULI KATIKA SIKU
Mfano wengi tunakula chakula kingi kulinganisha na shughuli tunazofanya.hii hupelekea kiwango kidogo kilichomeng'enywa kutumika na kingine kinachobaki kuhifadhiwa mwilini kama mafuta.
Hii pia imechangiwa na ongezeka la matumizi ya boda boda ,bajaji ,na magari kwa umbali mfupi. ambao umbali huo zamani tulikuwa tunatembea ila sasa tunatumia vyombo hivyo. kutembea umbali huo kungesaidia mmeng'enyo wa mafuta ya ziada katika miili yetu.
Tuongeze umbali tunaotembea kila siku. sio lazima uende kituoni au kwa dukani au sokoni kwa kutumia boda boda au bajaji
3.TUPIME AFYA ZETU MARA KWA MARA
Kila mwezi ,baada ya miezi 3 au 6 kulingana na hali yako ya kiuchumi.
FAIDA
Kugundua tatizo mapema hasa presha.
Kuzuia tatizo lisitokee na kuwa chronic
4. KUJIUNGA NA KLINIKI ZA MOYO
-Kupata elimu juu ya matatizo hayo
- Kuzingatia ushauri wa matumizi ya dawa za presha . wengi huacha dawa na kufanya presha zao ziwezisizodhibitiwa na kupelekea wao kupata kiharusi
- Kutonunua dawa za presha bila ushauri wa daktari
- Kuto acha matumizi ya dawa za presha bila ushauri wa daktari
Ukiwa na tatizo la presha ni muhimu kutumia dawa za kudhibiti presha kila siku ya maisha yako, na usipo zingatia hayo yaliyotajwa hapo juu. upo kwenye hatari ya kupata kiharusi.
5. HOSPITALI KUFANYA UFUATILIAJI
Kwa wagonjwa wa presha, na wahanga wa kiharusi pale ambapo wamegundulika na presha na wahanga wa kiharusi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani.
hii itapunguza vifo na ulemavu unaotokana na kiharusi
6. WATAALAM WAFIZIOTHERAPIA WAHUSIKE KATIKA DISCHARGE YA WAHANGA WA KIHARUSI.
Kwanza itambulike kuwa wataalma wa fiziotherapia ndio wahusika wa mazoezi tiba katika kuwarudishia watu nguvu za misuli na mwili baada ya kupooza.
Wafiziotherapia husaidia
¡ . Kumfundisha mgonjwa mbinu za kugeuka kitandani,kukaa na kuzuia ulemavu na ukakamavu wa viungo
¡¡. Kuwafundisha ndugu wa mgonjwa namna ya kumhudumia mgonjwa akiwa nyumbani - kumrisha,kumyoosha viungo,kumgeuza ,kumkalisha na kuzuia ulemavu
Hii itasaidia sana wagonjwa kupona kwa wepesi bila madhara ya kiharusi.
7. KUANZA MAZOEZI TIBA HARAKA SANA BAADA YA KUPATA KIHARUSI.
Kutokana na kukosa elimu kuhusiana na tatizo hili wahanga wengi hubaki majumbani bila matibabu yoyote hii uchangiwa pia na imani potofu wakizani kuwa wamelogwa la hasha ni matatizo fulani ya kiafya hupelekea tatizo hili.
Kadri mgonjwa anavyozidi kubaki nyumbani bila kuanza mazoezi tiba kwa mtaalamu wa fiziotherapia anazidi kuwa katika hatari ya kupata ulemavh wa kudumu au kifo.
8. OMBI KWA SERIKALI
Hospitali maalum za kutibu magonjwa ya moyo zianzishwe katika ngazi ya wilaya
mfano JKCI
HII ITASAIDIA
¡. Kupunguza vifo na ulemavu kutokana na ukaribu wa huduma kwa wahanga wa kiharusi
¡¡.Kupunguza msongamano kwenye hospitali kubwa ambao msongamano huo huchochea utoaji hafifu wa huduma kwa wahanga na kupelekea athari kama vifo na ulemavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment