Mme na Mke walibishana kila mmoja akijigamba kuwa ana rafiki mzuri. Ili kumaliza ubishi, wakaamua kuwapigia Marafiki zao kwa loud speaker.
Mme akampigia rafiki wa mkewe aitwae Anna akamuuliza.
Shemu mke wangu hajalala nyumbani, simu yake haipatikani labda unajua aliko.
ANNA:yaani hata shemu usipo sema nilijua tu toka zamani kwa maana alikuwa haishi kuniambia "mme wangu hana lolote, wengine waendelea yeye hamna kitu "kama ninge jua ndoa iko hivi nisinge kubali Kuolewa" nikuambie shemu bora amefanya vizuri akaondoka yaani huyo siyo mwanamke kabisa atakuua, kila Siku anauliza kuhusu mganga, shemu ukitaka kuoa uwage unauliza, mbona kuna mabinti wazuri tu, kwa mfano kuna huyu binti anae itwa Malta binti wa mama mdogo, ni Binti mtulivu kweli yuko tofauti kabisa na wengine, subiri nitakutumia namba yake, oa hata huyo kuliko huyo atakuua,:
Baadae mke nae akachua simu yake akampigia rafiki wa mmewe aitwae Michael akamuuliza, huku akiwa amesononeshwa na rafiki yake Anna vibaya mno.
Shemu kaka yako hajalala hapa nyumbani, hata simu yake haipatikani, labda unafahamu alipo.
MICHAEL AKAJIBU:
Aaaaa! Hahahahaa! Shemu usihofu kabisa, relax Shemu lake, ila naomba samahani kwa kuwa hatujakutalifu, tulilewa sana akalala hapa nyumbani kwangu,ameamuka kichwa kinamuuma, au nikupe uongee nae, "Oya shemu anakutafuta" aa shemu anadai kichwa bado kinauma so mtaongea baadae, usihofu shemu lake tunakuja hapo sasa hivi.

Baada ya kukata mme na mke wakatazamana wakaanza kucheka. Mara Michael akapiga simu kwa mme, mme akaweka loud speaker 🔊 Michael akasikika akisema.
Oya! Oya! Umelala wapi leo?. shemu amepiga simu anakutafuta kila kona, ila usihofu nisha rekebisha mambo, ukimaliza mambo yako njoo nikupeleke tukayajenge.
No comments:
Post a Comment