"Epuka kuweka furaha yako kwenye mikono ya watu, WATU HUBADILIKA... jitahidi chanzo cha furaha yako kitokane na wewe.
kwanza jione UNATOSHA, unapoanza kuhisi thamani yako haijakamilika bila fulani, umeshafeli.. kuna wengi wanaamini wao hawawezi kuwa wao bila kuwa kwenye vivuli vya wengine wanaoamini wao ndio wa maana na kujisahau ubora wao, huo ni utumwa mbaya utakaokukosesha furaha na kukufanya uwe nyuma ya wengine siku zote hata pale wanapokukataa kwa kudhani tu wao ndio wanakufanya wewe uwe wewe, na kwa namna hiyo fulani asipokuwepo kesho itakufanya ujishushe na kujiona hufai, na bila kujua hali ya namna hiyo (kujiona hutoshi) itakunyima furaha, hivyo Iepuke.
Kingine Tengeneza furaha kwa kuunda ratiba zako binafsi ambazo hazihitaji mwingine ili zikamilike, maana UNYONGE HUANZA UNAPOHITAJI MTU, na kumbuka watu hawapatikani muda wote unaowahitaji, watakapokosekana utanyong'onyea na kukosa furaha thats wrong.
Kingine unaposhindwa jambo/kuanguka ama kufeli kwenye kitu KUBALI, usijistress na maswali mengi, hatujaumbiwa kushinda muda wote, binaadamu tuko kwenye nyakati zote, hivyo kukubaliana na kuanguka ni kujitoa stress, unapogoma kukubali unajitafutia stress za lazima, kumbuka kufaulu na kufeli ni sehemu ya maisha.
Na zaidi MJUE MUNGU SANA, na hii inapaswa iwe ya kwanza, ukimjua MUNGU utadharau vingi sana vya kidunia, hautababaika na utaridhika na hali yoyote bila kukaa roho juu.
Kiufupi MSINGI WA FURAHA YAKO jitahidi uwe kwenye mikono yako, pamoja na matatizo na mitihani yote binaadamu tunahitaji furaha, maana furaha ndio msingi wa mengi hata ya kimaendeleo, Furaha huleta Amani, na aliekosa furaha hata mengine ya kawaida yanaweza kumshinda kufanya inavyotakiwa, hivyo pamoja na huzuni, matatizo na mitihani ya kibinaadamu jitahidi FURAHA ITAWALE.
Fahamu tu kuwa furaha hainunuliwi, lakini kizuri kuliko vyote furaha haitengenezwi kwa gharama kubwa, furaha ni wewe na misingi yako, na furaha unaweza KUIPATA AU KUIKOSA kutokana na MITAZAMO YAKO, na kubwa kuliko yote hakuna wa kukufurahisha ila WEWE."
No comments:
Post a Comment