Thursday, 4 April 2019

Wamalawi waomba kurudishwa nyumbani kwao


Baadhi ya raia wa Malawi wanaoishi mjini Durban nchini Afrika Kusini, wameomba kurudishwa nyumbani. Hatua hiyo inakuja baada ya kushambuliwa na raia wa Afrika Kusini, uvamizi wa raia hao wa kigeni ulisababisha wananchi wa Malawi wapatao 300 kuyakimbia makaazi yao.



Makaazi yao yalivamiwa na biashara zao kuharibiwa na wenyeji, suala ambalo limeikasirisha serikali ya Afrika Kusini na kuwataka maafisa wa usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua waliohusika.

Wimbi la raia wa Afrika Kusini kuwavamia raia wa kigeni kutoka mataifa mengine ya Afrika, limeendelea kuzua wasiwasi nchini humo.

Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni. Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!